Luka 24:16 - Swahili Revised Union Version Macho yao yakafumbwa wasimtambue. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Walimwona kwa macho, lakini hawakumtambua. Biblia Habari Njema - BHND Walimwona kwa macho, lakini hawakumtambua. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Walimwona kwa macho, lakini hawakumtambua. Neno: Bibilia Takatifu lakini macho yao yakazuiliwa ili wasimtambue. Neno: Maandiko Matakatifu lakini macho yao yakazuiliwa ili wasimtambue. BIBLIA KISWAHILI Macho yao yakafumbwa wasimtambue. |
Baada ya hayo akawatokea wawili miongoni mwao, akiwa na sura nyingine; nao walikuwa wakitembea njiani kwenda mashambani.
Akawaambia, Ni maneno gani haya mnayosemezana hivi mnapotembea? Wakasimama wamekunja nyuso zao.
Naye akiisha kusema hayo, akageuka nyuma, akamwona Yesu amesimama, asijue ya kuwa ni Yesu.