Heri watumwa wale, ambao bwana wao ajapo atawakuta wanakesha. Amin, nawaambieni, atajifunga na kuwakaribisha chakulani, atakuja na kuwahudumia.
Luka 22:16 - Swahili Revised Union Version kwa maana nawaambia ya kwamba siili tena hadi itakapotimizwa katika ufalme wa Mungu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Maana nawaambieni, sitaila tena hadi hapo itakapokamilika katika ufalme wa Mungu.” Biblia Habari Njema - BHND Maana nawaambieni, sitaila tena hadi hapo itakapokamilika katika ufalme wa Mungu.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Maana nawaambieni, sitaila tena hadi hapo itakapokamilika katika ufalme wa Mungu.” Neno: Bibilia Takatifu Kwa maana, nawaambia, sitaila tena Pasaka hadi itakapotimizwa katika ufalme wa Mungu.” Neno: Maandiko Matakatifu Kwa maana, nawaambia, sitaila tena Pasaka mpaka itakapotimizwa katika Ufalme wa Mwenyezi Mungu.” BIBLIA KISWAHILI kwa maana nawaambia ya kwamba siili tena hadi itakapotimizwa katika ufalme wa Mungu. |
Heri watumwa wale, ambao bwana wao ajapo atawakuta wanakesha. Amin, nawaambieni, atajifunga na kuwakaribisha chakulani, atakuja na kuwahudumia.
Basi aliposikia hayo mmojawapo wa wale walioketi chakulani pamoja naye alimwambia, Heri yule atakayekula mkate katika ufalme wa Mungu.
Maana nawaambia ya kwamba tangu sasa sinywi mazao ya mzabibu hadi ufalme wa Mungu utakapokuja.
mpate kula na kunywa mezani pangu katika ufalme wangu; na kuketi katika viti vya enzi, huku mkiyahukumu makabila kumi na mawili ya Israeli.
Msikitendee kazi chakula chenye kuharibika, bali chakula kidumucho hata uzima wa milele; ambacho Mwana wa Adamu atawapa, kwa sababu huyo ndiye aliyetiwa mhuri na Baba, yaani, Mungu.
si kwa watu wote, bali kwa mashahidi waliokuwa wamekwisha kuchaguliwa na Mungu, ndio sisi, tuliokula na kunywa pamoja naye baada ya kufufuka kwake kutoka kwa wafu.
Naye akaniambia, Andika, Heri walioalikwa katika karamu ya arusi ya Mwana-kondoo. Akaniambia, Maneno haya ni maneno ya kweli ya Mungu.