Luka 2:47 - Swahili Revised Union Version Nao wote waliomsikia walistaajabia fahamu zake na majibu yake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Wote waliosikia maneno yake walistaajabia akili yake na majibu yake ya hekima. Biblia Habari Njema - BHND Wote waliosikia maneno yake walistaajabia akili yake na majibu yake ya hekima. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Wote waliosikia maneno yake walistaajabia akili yake na majibu yake ya hekima. Neno: Bibilia Takatifu Wote waliomsikia walistaajabishwa na uwezo wake mkubwa wa kuelewa, na majibu aliyoyatoa. Neno: Maandiko Matakatifu Wote waliomsikia walistaajabishwa na uwezo wake mkubwa wa kuelewa, na majibu aliyoyatoa. BIBLIA KISWAHILI Nao wote waliomsikia walistaajabia fahamu zake na majibu yake. |
Na alipofika mji wa kwao, akawafundisha katika sinagogi lao, hata wakashangaa, wakasema, Huyu amepata wapi hekima hii na miujiza hii?
Wakashangaa mno kwa mafundisho yake; kwa maana alikuwa akiwafundisha kama mtu mwenye mamlaka, wala si kama waandishi.
Wakuu wa makuhani na waandishi wakapata habari wakatafuta jinsi ya kumwangamiza; maana walimwogopa, kwa sababu mkutano wote walishangazwa na mafundisho yake.
Na ilipokuwa sabato, alianza kufundisha katika sinagogi; wengi waliposikia wakashangaa, wakisema, Huyu ameyapata wapi haya? Na, Ni hekima gani hii aliyopewa huyu? Na, Ni nini miujiza hii mikubwa inayotendeka kwa mikono yake?
Ikawa baada ya siku tatu wakamwona hekaluni, ameketi katikati ya waalimu, akiwasikiliza na kuwauliza maswali.
Wakamshuhudia wote, wakiyastaajabia maneno ya neema yaliyotoka kinywani mwake, wakasema, Huyu siye mwana wa Yusufu?