Akaandaliwa chakula, lakini akasema, Sili mpaka niseme kwanza maneno yangu. Akamwambia, Haya, sema.
Luka 10:4 - Swahili Revised Union Version Msichukue mfuko, wala mkoba, wala viatu; wala msimwamkie mtu njiani. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Msichukue mfuko wa fedha, mkoba, wala viatu; msimsalimu mtu yeyote njiani. Biblia Habari Njema - BHND Msichukue mfuko wa fedha, mkoba, wala viatu; msimsalimu mtu yeyote njiani. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Msichukue mfuko wa fedha, mkoba, wala viatu; msimsalimu mtu yeyote njiani. Neno: Bibilia Takatifu Msichukue mkoba, wala mfuko, wala viatu, na msimsalimu mtu yeyote njiani. Neno: Maandiko Matakatifu Msichukue mkoba, wala mfuko, wala viatu, na msimsalimu mtu yeyote njiani. BIBLIA KISWAHILI Msichukue mfuko, wala mkoba, wala viatu; wala msimwamkie mtu njiani. |
Akaandaliwa chakula, lakini akasema, Sili mpaka niseme kwanza maneno yangu. Akamwambia, Haya, sema.
Naye akawaambia, Msinikawilishe, mradi BWANA amefanikisha njia yangu; nipeni ruhusa niende kwa bwana wangu.
Akatandika punda, akamwambia mtumishi wake, Mwendeshe, twendelee mbele. Usinipunguzie mwendo, nisipokuambia.
Ndipo Elisha akamwambia Gehazi, Jikaze viuno, ukachukue fimbo yangu mkononi mwako, ukaende zako; ukikutana na mtu, usimsalimu; na mtu akikusalimu, usimjibu; ukaweke fimbo yangu juu ya uso wa mtoto.
Akawaita wale Kumi na Wawili, akaanza kuwatuma wawili wawili, akawapa amri juu ya pepo wachafu;
Akawauliza, Je! Hapo nilipowatuma hamna mfuko, wala mkoba, wala viatu, mlipungukiwa na kitu? Wakasema, La!
Tena Daudi akamwambia Ahimeleki, Na hapa chini ya mkono wako, je! Hapana mkuki, au upanga? Kwa maana sikuleta upanga, wala silaha zangu, kwa sababu ile shughuli ya mfalme ilitaka haraka.