Luka 1:67 - Swahili Revised Union Version Na Zakaria, baba yake, akajazwa Roho Mtakatifu, akatabiri, akisema, Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Zakaria, baba yake mtoto, akajazwa Roho Mtakatifu, akatamka unabii huu: Biblia Habari Njema - BHND Zakaria, baba yake mtoto, akajazwa Roho Mtakatifu, akatamka unabii huu: Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Zakaria, baba yake mtoto, akajazwa Roho Mtakatifu, akatamka unabii huu: Neno: Bibilia Takatifu Zakaria, baba yake, akajazwa na Roho Mtakatifu wa Mungu, naye akatoa unabii, akisema: Neno: Maandiko Matakatifu Zekaria, baba yake, akajazwa na Roho wa Mwenyezi Mungu, naye akatoa unabii, akisema: BIBLIA KISWAHILI Na Zakaria, baba yake, akajazwa Roho Mtakatifu, akatabiri, akisema, |
Hata itakuwa, baada ya hayo, ya kwamba nitamimina roho yangu juu ya wote wenye mwili; na wana wenu, wa kiume na wa kike, watatabiri, wazee wenu wataota ndoto, na vijana wenu wataona maono;
Ndipo BWANA akashuka ndani ya wingu, akanena naye, akatwaa sehemu ya roho iliyokuwa juu ya Musa, akaitia juu ya wale wazee sabini; ikawa, roho hiyo ilipowashukia, wakatabiri, lakini hawakufanya hivyo tena.
Kwa sababu atakuwa mkuu mbele za Bwana; hatakunywa divai wala kileo; naye atajazwa Roho Mtakatifu hata tangu tumboni mwa mamaye.
Ikawa Elisabeti aliposikia kule kuamkia kwake Mariamu, kitoto kichanga kikaruka ndani ya tumbo lake; Elisabeti akajazwa Roho Mtakatifu;
Wote wakajazwa Roho Mtakatifu, wakaanza kusema kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowajalia kutamka.
Anania akaenda zake, akaingia mle nyumbani; akamwekea mikono akisema, Ndugu Sauli, Bwana amenituma, Yesu, yeye aliyekutokea katika njia uliyoijia, upate kuona tena, ukajazwe Roho Mtakatifu.
Maana unabii haukuletwa popote kwa mapenzi ya mwanadamu; bali wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu, wakiongozwa na Roho Mtakatifu.