Biblia ya mtandaoni

Matangazo


Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya




Kutoka 1:9 - Swahili Revised Union Version

Akawaambia watu wake, Angalieni, watu wa wana wa Israeli ni wengi tena wana nguvu kuliko sisi.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Naye akawaambia watu wake, “Tazameni jinsi Waisraeli walivyo wengi na wenye nguvu kuliko sisi.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Naye akawaambia watu wake, “Tazameni jinsi Waisraeli walivyo wengi na wenye nguvu kuliko sisi.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Naye akawaambia watu wake, “Tazameni jinsi Waisraeli walivyo wengi na wenye nguvu kuliko sisi.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Akawaambia watu wake, “Tazameni, Waisraeli wamekuwa wengi mno kwa idadi kuliko sisi.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Akawaambia watu wake, “Tazameni, Waisraeli wamekuwa wengi mno kwa idadi kutuliko sisi.

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Akawaambia watu wake, Angalieni, watu wa wana wa Israeli ni wengi tena wana nguvu kuliko sisi.

Tazama sura
Tafsiri zingine



Kutoka 1:9
12 Marejeleo ya Msalaba  

Abimeleki akamwambia Isaka, Utoke kwetu, maana wewe una nguvu sana kuliko sisi.


Akasema, Mimi ni Mungu, Mungu wa baba yako, usiogope kushuka mpaka Misri; maana nitakufanya uwe taifa kubwa huko.


Kwani hasira humwua mtu mpumbavu, Nao wivu humwua mjinga.


Kisha Farao akasema, Tazameni, watu wa nchi sasa ni wengi, nanyi mnawapumzisha, wasichukue mizigo yao.


Utukufu wa mfalme ni wingi wa watu wake; Bali uchache wa watu ni uharibifu wa mkuu wao.


Ghadhabu ni kali, na hasira ni gharika; Lakini ni nani awezaye kusimama mbele ya wivu.


Tena nikagundua kuwa juhudi zote, na ustadi wote katika kazi, hutokana na mtu kumwonea mwingine wivu. Hayo nayo ni ubatili na kufukuza upepo.


Maana hapo zamani sisi nasi tulikuwa hatuna akili, tulikuwa waasi, tumedanganywa, huku tukitumikia tamaa na anasa za namna nyingi, tukiishi katika uovu na husuda, tukichukiza na kuchukiana.


Au mwadhani ya kwamba Maandiko yasema bure? Huyo Roho akaaye ndani yetu hututamani kiasi cha kuona wivu?