Wakatoka wakati wa adhuhuri. Lakini Ben-hadadi alikuwa akinywa hata kulewa mabandani, yeye na wale wafalme thelathini na wawili waliomsaidia.
Isaya 5:22 - Swahili Revised Union Version Ole wao walio hodari kunywa kileo chenye nguvu, na walio hodari wa kuchanganya vileo; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Ole wao mabingwa wa kunywa divai, hodari sana wa kuchanganya vileo. Biblia Habari Njema - BHND Ole wao mabingwa wa kunywa divai, hodari sana wa kuchanganya vileo. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Ole wao mabingwa wa kunywa divai, hodari sana wa kuchanganya vileo. Neno: Bibilia Takatifu Ole wao walio mashujaa kwa kunywa mvinyo, nao walio hodari katika kuchanganya vileo, Neno: Maandiko Matakatifu Ole wao walio mashujaa kwa kunywa mvinyo, nao walio hodari katika kuchanganya vileo, BIBLIA KISWAHILI Ole wao walio hodari kunywa kileo chenye nguvu, na walio hodari wa kuchanganya vileo; |
Wakatoka wakati wa adhuhuri. Lakini Ben-hadadi alikuwa akinywa hata kulewa mabandani, yeye na wale wafalme thelathini na wawili waliomsaidia.
Nawe usipokee rushwa; kwani hiyo rushwa huwapofusha macho hao waonao, na kuyapotoa maneno ya wenye haki.
Ni nani apigaye, Yowe? Ni nani aliaye, Ole? Ni nani mwenye ugomvi? Ni nani mwenye mguno? Ni nani aliye na majeraha yasiyo na sababu? Ni nani aliye na macho mekundu?
Ee Lemueli, kunywa mvinyo hakuwafai wafalme, hakuwafai wafalme; Wala haifai wakuu waseme, Kiko wapi kileo?
na kumbe! Furaha, na kuchekelea, na kuchinja ng'ombe, na kuchinja kondoo, na kula nyama, na kunywa mvinyo; tule, tunywe, kwa maana kesho tutakufa.
Lakini hawa nao wamekosa kwa divai, wamepotea kwa kileo; kuhani na nabii wamekosa kwa kileo, wamemezwa kwa divai, wamepotea kwa kileo; hukosa katika maono, hujikwaa katika hukumu.
Ole wao waamkao asubuhi na mapema, wapate kufuata kileo; wakishinda sana hadi usiku wa manane mpaka mvinyo imewaka kama moto ndani yao!
Husema, Njooni, nitaleta divai, Na tunywe sana kileo; Na kesho itakuwa kama leo, Sikukuu kupita kiasi.
Ole wake yeye ampaye jirani yake kileo, wewe utiaye sumu yako, na kumlevya pia, ili kuutazama uchi wao!