Isaya 40:8 - Swahili Revised Union Version Majani yakauka, ua lanyauka; Bali neno la Mungu wetu litasimama milele. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Majani hunyauka na ua hufifia, lakini neno la Mungu wetu ladumu milele.” Biblia Habari Njema - BHND Majani hunyauka na ua hufifia, lakini neno la Mungu wetu ladumu milele.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Majani hunyauka na ua hufifia, lakini neno la Mungu wetu ladumu milele.” Neno: Bibilia Takatifu Majani hunyauka na maua huanguka, lakini neno la Mungu wetu ladumu milele.” Neno: Maandiko Matakatifu Majani hunyauka na maua huanguka, lakini neno la Mungu wetu ladumu milele.” BIBLIA KISWAHILI Majani yakauka, ua lanyauka; Bali neno la Mungu wetu litasimama milele. |
Tena kuhusu habari zangu, hili ndilo agano langu nao, asema BWANA; roho yangu iliyo juu yako, na maneno yangu niliyoyatia kinywani mwako, hayataondoka kinywani mwako, wala kinywani mwa wana wako, wala kinywani mwa wajukuu wako, asema BWANA, tangu leo na hata milele.
Na hii ndiyo itakayokuwa ishara kwenu, asema BWANA, kwamba mimi nitawaadhibu ninyi mahali hapa, mpate kujua ya kuwa maneno yangu yatasimama juu yenu, kuwaletea mabaya bila shaka;
Lakini maneno yangu, na amri zangu nilizowaagiza hao manabii, watumishi wangu, je, Hazikuwapata baba zenu? Nao wakatubu na kusema, BWANA wa majeshi ametutenda kulingana na njia zetu, na matendo yetu, kama alivyokusudia kutenda.
Mungu si mtu, aseme uongo; Wala si mwanadamu, ajute; Iwapo amesema, hatalitenda? Iwapo amenena, hatalitimiza?
Kwa maana, amin, nawaambia, Mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka, yodi moja wala nukta moja ya torati haitaondoka, hata yote yatimie.
Ikiwa aliwaita miungu wale waliojiwa na neno la Mungu; (na maandiko hayawezi kutanguka);
Basi mkutano wakamjibu, Sisi tumesikia katika torati ya kwamba Kristo adumu hata milele; nawe wasemaje ya kwamba imempasa Mwana wa Adamu kuinuliwa? Huyu Mwana wa Adamu ni nani?
Bali Neno la Bwana hudumu hata milele. Na neno hilo ni neno lile jema lililohubiriwa kwenu.