Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Isaya 40:7 - Swahili Revised Union Version

7 Majani yakauka, ua lanyauka; Kwa sababu pumzi ya BWANA yapita juu yake. Hakika watu ni majani.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

7 Majani hunyauka na ua hufifia, Mwenyezi-Mungu avumishapo upepo juu yake. Hakika binadamu ni kama majani.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

7 Majani hunyauka na ua hufifia, Mwenyezi-Mungu avumishapo upepo juu yake. Hakika binadamu ni kama majani.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

7 Majani hunyauka na ua hufifia, Mwenyezi-Mungu avumishapo upepo juu yake. Hakika binadamu ni kama majani.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

7 Majani hunyauka na maua huanguka, kwa sababu pumzi ya Mwenyezi Mungu huyapuliza. Hakika wanadamu ni majani.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

7 Majani hunyauka na maua huanguka, kwa sababu pumzi ya bwana huyapuliza. Hakika wanadamu ni majani.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

7 Majani yakauka, ua lanyauka; Kwa sababu pumzi ya BWANA yapita juu yake. Hakika watu ni majani.

Tazama sura Nakili




Isaya 40:7
15 Marejeleo ya Msalaba  

Yeye huchanua kama vile ua, kisha hukatwa; Hukimbia kama kivuli, wala hakai kamwe.


Kwa pumzi za Mungu huangamia. Na kwa kuvuma kwa hasira zake humalizika.


Pumzi zake huwasha makaa, Na miali ya moto hutoka kinywani mwake.


Moyo wangu umepigwa kama majani na kukauka, Naam, ninasahau kula chakula changu.


Mwanadamu siku zake zi kama majani; Kama ua la kondeni ndivyo anavyostawi.


Maana upepo hupita juu yake, na kutoweka! Lisionekane mahali lilipokuwa tena.


Wawafutilia wanadamu mbali kama ndoto, wao ni kama majani yameayo asubuhi.


Asubuhi yachipuka na kumea, Jioni yakatika na kukauka.


bali kwa haki atawahukumu maskini, naye atawaonya wanyenyekevu wa dunia kwa adili; naye ataipiga dunia kwa fimbo ya kinywa chake, na kwa pumzi ya midomo yake atawaua wabaya.


Ndiyo sababu wenyeji wao wakawa hawana nguvu, na kufadhaika, na kuhangaika, wakawa kama majani ya mashamba, kama miche mibichi, kama majani juu ya madari, kama shamba la ngano kabla haijaiva.


Naam, hawakupandwa; hawakutiwa katika ardhi kama mbegu; naam, shina lao halikutia mizizi katika ardhi; tena awapuzia tu, wakanyauka, upepo wa kisulisuli wawaondoa kama mabua makavu.


Mimi, naam, mimi, ndimi niwafarijiye; wewe u nani hata ukamwogopa mtu atakayekufa, na mwanadamu atakayefanywa kuwa kama majani?


Mlitazamia vingi, kumbe vikatokea vichache; tena mlipovileta nyumbani nikavipeperusha mbali. Ni kwa sababu gani? Asema BWANA wa majeshi. Ni kwa sababu yumba yangu imebaki kuwa gofu la nyumba, wakati ambapo kila mmoja wenu anakimbilia nyumbani kwake.


bali tajiri kwa kuwa ameshushwa; kwa maana atatoweka kama ua la majani.


Maana jua huchomoza kwa joto kali, huyakausha majani; ua lake huanguka, uzuri wa umbo lake hupotea; vivyo hivyo naye tajiri atanyauka katika njia zake.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo