Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Isaya 59:21 - Swahili Revised Union Version

21 Tena kuhusu habari zangu, hili ndilo agano langu nao, asema BWANA; roho yangu iliyo juu yako, na maneno yangu niliyoyatia kinywani mwako, hayataondoka kinywani mwako, wala kinywani mwa wana wako, wala kinywani mwa wajukuu wako, asema BWANA, tangu leo na hata milele.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

21 Mwenyezi-Mungu asema: “Mimi nafanya nanyi agano hili: Roho yangu niliyowajazeni, maneno niliyoyaweka mdomoni mwenu, hayataondoka kwenu kamwe, wala kwa watoto na wajukuu zenu, tangu sasa na hata milele.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

21 Mwenyezi-Mungu asema: “Mimi nafanya nanyi agano hili: Roho yangu niliyowajazeni, maneno niliyoyaweka mdomoni mwenu, hayataondoka kwenu kamwe, wala kwa watoto na wajukuu zenu, tangu sasa na hata milele.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

21 Mwenyezi-Mungu asema: “Mimi nafanya nanyi agano hili: Roho yangu niliyowajazeni, maneno niliyoyaweka mdomoni mwenu, hayataondoka kwenu kamwe, wala kwa watoto na wajukuu zenu, tangu sasa na hata milele.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

21 “Bali mimi, hili ndilo agano langu nao,” asema Mwenyezi Mungu. “Roho wangu Mtakatifu, aliye juu yenu, na maneno yangu niliyoyaweka vinywani vyenu, havitaondoka vinywani mwenu, wala kutoka vinywani mwa watoto wenu, wala kutoka vinywani mwa wazao wao, kuanzia sasa na hata milele,” asema Mwenyezi Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

21 “Kwa habari yangu mimi, hili ndilo agano langu nao,” asema bwana. “Roho wangu, aliye juu yenu, na maneno yangu ambayo nimeyaweka katika vinywa vyenu, havitaondoka vinywani mwenu, wala kutoka vinywani mwa watoto wenu, wala kutoka vinywani mwa wazao wao, kuanzia sasa na hata milele,” asema bwana.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

21 Tena kuhusu habari zangu, hili ndilo agano langu nao, asema BWANA; roho yangu iliyo juu yako, na maneno yangu niliyoyatia kinywani mwako, hayataondoka kinywani mwako, wala kinywani mwa wana wako, wala kinywani mwa wajukuu wako, asema BWANA, tangu leo na hata milele.

Tazama sura Nakili




Isaya 59:21
36 Marejeleo ya Msalaba  

Usiliondoe neno la kweli kinywani mwangu kamwe, Maana nimezingojea hukumu zako.


Nawe utasema naye, na kuyatia maneno kinywani mwake; nami nitakuwa pamoja na kinywa chako, na pamoja na kinywa chake, na kuwafundisheni mtakayofanya.


Zifunge katika vidole vyako; Ziandike juu ya kibao cha moyo wako.


hata roho itakapomwagwa juu yetu kutoka juu; hata jangwa litakapokuwa shamba lizaalo sana; nalo shamba lizaalo sana litakapohesabiwa kuwa msitu.


Majani yakauka, ua lanyauka; Bali neno la Mungu wetu litasimama milele.


Tazama mtumishi wangu nimtegemezaye; mteule wangu, ambaye nafsi yangu imependezwa naye; nimetia roho yangu juu yake; naye atawatolea mataifa hukumu.


Kwa maana nitamimina maji juu yake aliye na kiu, na vijito vya maji juu ya mahali pakavu; nitamwaga roho yangu juu ya wazao wako, na baraka yangu juu yao utakaowazaa;


BWANA asema hivi, Wakati uliokubalika nimekujibu, na siku ya wokovu nimekusaidia; nami nitakuhifadhi, nitakutoa uwe agano la watu hawa, ili kuiinua nchi hii, na kuwarithisha urithi uliokuwa ukiwa;


BWANA wa majeshi ndilo jina lake. Nami nimetia maneno yangu kinywani mwako, nami nimekusitiri katika kivuli cha mkono wangu, ili nizipande mbingu, na kuiweka misingi ya dunia, na kuuambia Sayuni, Ninyi ni watu wangu.


Maana milima itaondoka, na vilima vitaondolewa; bali wema wangu hautaondoka kwako, wala agano langu la amani halitaondolewa; asema BWANA akurehemuye.


ndivyo litakavyokuwa neno langu, litokalo katika kinywa changu; halitanirudia bure, bali litatimiza mapenzi yangu, nalo litafanikiwa katika mambo yale niliyolituma.


Tegeni masikio yenu, na kunijia; Sikieni, na nafsi zenu zitaishi; Nami nitafanya nanyi agano la milele, Naam, rehema za Daudi zilizo imara.


Mimi nayaumba matunda ya midomo; Amani, amani, kwake yeye aliye mbali, na kwake yeye aliye karibu; asema BWANA; nami nitamponya.


Kama vile mbingu mpya na nchi mpya, nitakazofanya, zitakavyokaa mbele zangu, asema BWANA, ndivyo uzao wenu na jina lenu litakavyokaa.


Ndipo BWANA akaunyosha mkono wake, akanigusa kinywa changu; BWANA akaniambia, Tazama, nimetia maneno yangu kinywani mwako;


Wala mimi sikumjua; lakini yeye aliyenituma kubatiza kwa maji, huyo aliniambia, Yeye ambaye utamwona Roho akishuka na kukaa juu yake, huyo ndiye abatizaye kwa Roho Mtakatifu.


Kwa kuwa maneno uliyonipa nimewapa wao; nao wakayapokea, wakajua hakika ya kuwa nilitoka kwako, wakasadiki ya kwamba wewe ndiwe uliyenituma.


Kwa kuwa yeye aliyetumwa na Mungu huyanena maneno ya Mungu; kwa sababu hamtoi Roho kwa kipimo.


lakini yeyote atakayekunywa maji yale nitakayompa mimi hataona kiu milele; bali yale maji nitakayompa yatakuwa ndani yake chemchemi ya maji, yakibubujikia uzima wa milele.


Na neno hilo alilisema kuhusu Roho, ambaye wale wamwaminio watampokea baadaye; kwa maana Roho alikuwa hajaja, kwa sababu Yesu alikuwa hajatukuzwa.


Niliyoyaona kwa Baba ndiyo niyanenayo; nanyi vivyo hivyo mliyoyasikia kwa baba yenu ndiyo myatendayo.


Na hili ndilo agano langu nao, Nitakapowaondolea dhambi zao.


Lakini ikiwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu, ninyi hamwufuati mwili; bali mwaifuata roho. Lakini mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa Kristo, huyo si wake.


je! Huduma ya roho haitazidi kuwa katika utukufu?


Hili ni agano nitakaloagana nao baada ya siku zile, anena Bwana, Nitatia sheria zangu mioyoni mwao, Na katika fikira zao nitaziandika; ndipo anenapo,


Tufuate:

Matangazo


Matangazo