Isaya 38:10 - Swahili Revised Union Version Nilisema, Katika usitawi wa siku zangu nitakwenda kuingia malango ya kuzimu; Nimenyimwa mabaki ya miaka yangu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema “Nilisema: Nikiwa mbichi kabisa, inanibidi niage dunia. Mimi nimepangiwa kwenda kuzimu siku zote zilizonibakia. Biblia Habari Njema - BHND “Nilisema: Nikiwa mbichi kabisa, inanibidi niage dunia. Mimi nimepangiwa kwenda kuzimu siku zote zilizonibakia. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza “Nilisema: nikiwa mbichi kabisa, inanibidi niage dunia. Mimi nimepangiwa kwenda kuzimu siku zote zilizonibakia. Neno: Bibilia Takatifu Nilisema, “Katika ustawi wa maisha yangu, je, ni lazima nipite katika malango ya mauti, na kupokonywa miaka yangu iliyobaki?” Neno: Maandiko Matakatifu Nilisema, “Katika ustawi wa maisha yangu, je, ni lazima nipite katika malango ya mauti, na kupokonywa miaka yangu iliyobaki?” BIBLIA KISWAHILI Nilisema, Katika usitawi wa siku zangu nitakwenda kuingia malango ya kuzimu; Nimenyimwa mabaki ya miaka yangu. |
Nitasema, Ee Mungu wangu, usiniondoe katikati ya siku zangu; Miaka yako ni tangu kizazi hata kizazi.
Mpendeni BWANA, Ninyi nyote mlio watauwa wake. BWANA huwahifadhi waaminifu, Bali humlipiza mwenye kiburi ipasavyo.
Lolote mkono wako utakalolipata kulifanya, ulifanye kwa nguvu zako; kwa kuwa hakuna kazi, wala shauri, wala maarifa, wala hekima, huko kuzimu uendako wewe.
Siku hizo Hezekia aliugua, akawa karibu kufa; na Isaya nabii, mwana wa Amozi, akaenda kwa mfalme, akamwambia, BWANA asema hivi, Tengeneza mambo ya nyumba yako; maana utakufa, wala hutapona.
Haya ndiyo maandiko ya Hezekia, mfalme wa Yuda, alipokuwa mgonjwa, naye akapona ugonjwa wake.
Nilishuka hata pande za chini za milima; Hiyo nchi ambayo mapingo yake yanafunga hata milele; Lakini umeipandisha nafsi yangu kutoka humo shimoni, Ee BWANA, Mungu wangu,
Naam, sisi wenyewe tulikuwa na hukumu ya mauti katika nafsi zetu ili tusijitumainie nafsi zetu, bali tumtumaini Mungu, awafufuaye wafu,