Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

Isaya 38:1 - Swahili Revised Union Version

1 Siku hizo Hezekia aliugua, akawa karibu kufa; na Isaya nabii, mwana wa Amozi, akaenda kwa mfalme, akamwambia, BWANA asema hivi, Tengeneza mambo ya nyumba yako; maana utakufa, wala hutapona.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

1 Wakati huo, mfalme Hezekia aliugua sana karibu kufa. Ndipo nabii Isaya mwana wa Amozi, akamwendea, akamwambia, “Hivi ndivyo anavyosema Mwenyezi-Mungu: Panga mambo yako sawasawa katika nyumba yako kwa kuwa utakufa, hutapona.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

1 Wakati huo, mfalme Hezekia aliugua sana karibu kufa. Ndipo nabii Isaya mwana wa Amozi, akamwendea, akamwambia, “Hivi ndivyo anavyosema Mwenyezi-Mungu: Panga mambo yako sawasawa katika nyumba yako kwa kuwa utakufa, hutapona.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

1 Wakati huo, mfalme Hezekia aliugua sana karibu kufa. Ndipo nabii Isaya mwana wa Amozi, akamwendea, akamwambia, “Hivi ndivyo anavyosema Mwenyezi-Mungu: Panga mambo yako sawasawa katika nyumba yako kwa kuwa utakufa, hutapona.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

1 Katika siku hizo Hezekia akaugua, naye akawa karibu kufa. Nabii Isaya mwana wa Amozi akaenda kwake na kumwambia, “Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: Tengeneza mambo ya nyumba yako, kwa sababu utakufa, hutapona.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

1 Katika siku hizo Hezekia akaugua, naye akawa karibu kufa. Nabii Isaya mwana wa Amozi akaenda kwake na kumwambia, “Hili ndilo asemalo bwana: Tengeneza mambo ya nyumba yako, kwa sababu utakufa, hutapona.”

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

1 Siku hizo Hezekia aliugua, akawa karibu kufa; na Isaya nabii, mwana wa Amozi, akaenda kwa mfalme, akamwambia, BWANA asema hivi, Tengeneza mambo ya nyumba yako; maana utakufa, wala hutapona.

Tazama sura Nakili

Isaya 38:1
16 Marejeleo ya Msalaba  

Akasema, Mtoto alipokuwa hai, nilifunga, nikalia; kwa maana nilisema, Ni nani ajuaye kama BWANA atanihurumia, mtoto apate kuishi?

Naye Ahithofeli alipoona ya kuwa ushauri wake haukufuatwa, akatandika punda wake, akaondoka, akaenda nyumbani kwake, mjini mwake, akaitengeneza nyumba yake, akajinyonga; akafa, akazikwa kaburini mwa babaye.

Katika siku hizo Hezekia akaugua akawa katika hatari ya kufa; akamwomba BWANA; naye akasema naye, akampa ishara.

Lolote mkono wako utakalolipata kulifanya, ulifanye kwa nguvu zako; kwa kuwa hakuna kazi, wala shauri, wala maarifa, wala hekima, huko kuzimu uendako wewe.

Haya ni maono ya Isaya, mwana wa Amozi aliyoyaona kuhusu Yuda na Yerusalemu, siku za Uzia, Yothamu, Ahazi na Hezekia, wafalme wa Yuda.

Akamtuma Eliakimu aliyekuwa msimamizi wa nyumba yake na Shebna, mwandishi, na wazee wa makuhani, wakiwa wamejivika nguo za magunia, waende kwa Isaya nabii, mwana wa Amozi.

Ndipo Isaya, mwana wa Amozi, akatuma ujumbe kwa Hezekia, akisema, BWANA, Mungu wa Israeli, asema hivi, Kwa kuwa umeniomba juu ya Senakeribu, mfalme wa Ashuru,

Mungu akaona matendo yao, ya kuwa wameiacha njia yao mbaya. Basi Mungu akalighairi neno lile baya, ambalo alisema atawatenda; asilitende.

Yona akaanza kuuingia mji mwendo wa siku moja, akapaza sauti yake, akasema, Baada ya siku arubaini Ninawi utaangamizwa.

Ikawa siku zile akaugua, akafa; wakati walipokwisha kumwosha, wakamweka ghorofani.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo