Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Isaya 38:10 - Swahili Revised Union Version

10 Nilisema, Katika usitawi wa siku zangu nitakwenda kuingia malango ya kuzimu; Nimenyimwa mabaki ya miaka yangu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

10 “Nilisema: Nikiwa mbichi kabisa, inanibidi niage dunia. Mimi nimepangiwa kwenda kuzimu siku zote zilizonibakia.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

10 “Nilisema: Nikiwa mbichi kabisa, inanibidi niage dunia. Mimi nimepangiwa kwenda kuzimu siku zote zilizonibakia.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

10 “Nilisema: nikiwa mbichi kabisa, inanibidi niage dunia. Mimi nimepangiwa kwenda kuzimu siku zote zilizonibakia.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

10 Nilisema, “Katika ustawi wa maisha yangu, je, ni lazima nipite katika malango ya mauti, na kupokonywa miaka yangu iliyobaki?”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

10 Nilisema, “Katika ustawi wa maisha yangu, je, ni lazima nipite katika malango ya mauti, na kupokonywa miaka yangu iliyobaki?”

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

10 Nilisema, Katika usitawi wa siku zangu nitakwenda kuingia malango ya kuzimu; Nimenyimwa mabaki ya miaka yangu.

Tazama sura Nakili




Isaya 38:10
12 Marejeleo ya Msalaba  

Nguvu zangu ni zipi, hata ningoje? Na mwisho wangu ni nini, hata nisubiri?


Kumbuka ya kwamba maisha yangu ni upepo; Jicho langu halitaona mema tena.


Nitasema, Ee Mungu wangu, usiniondoe katikati ya siku zangu; Miaka yako ni tangu kizazi hata kizazi.


Hapo mwanzo uliutia msingi wa nchi, Na mbingu ni kazi ya mikono yako.


Nafsi zao zachukia kila namna ya chakula, Wameyakaribia malango ya mauti.


Mpendeni BWANA, Ninyi nyote mlio watauwa wake. BWANA huwahifadhi waaminifu, Bali humlipiza mwenye kiburi ipasavyo.


Lolote mkono wako utakalolipata kulifanya, ulifanye kwa nguvu zako; kwa kuwa hakuna kazi, wala shauri, wala maarifa, wala hekima, huko kuzimu uendako wewe.


Siku hizo Hezekia aliugua, akawa karibu kufa; na Isaya nabii, mwana wa Amozi, akaenda kwa mfalme, akamwambia, BWANA asema hivi, Tengeneza mambo ya nyumba yako; maana utakufa, wala hutapona.


Haya ndiyo maandiko ya Hezekia, mfalme wa Yuda, alipokuwa mgonjwa, naye akapona ugonjwa wake.


Nilishuka hata pande za chini za milima; Hiyo nchi ambayo mapingo yake yanafunga hata milele; Lakini umeipandisha nafsi yangu kutoka humo shimoni, Ee BWANA, Mungu wangu,


Naam, sisi wenyewe tulikuwa na hukumu ya mauti katika nafsi zetu ili tusijitumainie nafsi zetu, bali tumtumaini Mungu, awafufuaye wafu,


Tufuate:

Matangazo


Matangazo