Isaya 28:5 - Swahili Revised Union Version Katika siku ile BWANA wa majeshi atakuwa ni taji la fahari, na kilemba cha uzuri, kwa mabaki ya watu wake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Siku ile Mwenyezi-Mungu wa majeshi atakuwa taji tukufu, kama kilemba kizuri kwa watu wake watakaobaki hai. Biblia Habari Njema - BHND Siku ile Mwenyezi-Mungu wa majeshi atakuwa taji tukufu, kama kilemba kizuri kwa watu wake watakaobaki hai. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Siku ile Mwenyezi-Mungu wa majeshi atakuwa taji tukufu, kama kilemba kizuri kwa watu wake watakaobaki hai. Neno: Bibilia Takatifu Katika siku ile, Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni atakuwa taji la utukufu, taji zuri la maua kwa mabaki ya watu wake. Neno: Maandiko Matakatifu Katika siku ile, bwana Mwenye Nguvu Zote atakuwa taji la utukufu, taji zuri la maua kwa mabaki ya watu wake. BIBLIA KISWAHILI Katika siku ile BWANA wa majeshi atakuwa ni taji la fahari, na kilemba cha uzuri, kwa mabaki ya watu wake. |
Itakuwako njia kuu kwa mabaki ya watu wake watakaobaki, watokao Ashuru, kama vile ilivyokuwako kwa Israeli, katika siku ile waliyotoka katika nchi ya Misri.
Toka pande za mwisho wa dunia tumesikia nyimbo, Atukuzwe mwenye haki. Ndipo niliposema, Kukonda kwangu! Kukonda kwangu! Ole wangu! Watenda hila wametenda hila, naam, watendao hila wametenda hila sana.
Tena itakuwa ya kwamba yeye aliyebaki katika Sayuni, na yeye aliyeachwa ndani ya Yerusalemu, ataitwa mtakatifu; yaani, kila mmoja aliyeandikwa miongoni mwa hao walio hai ndani ya Yerusalemu;
Utawapepeta, na upepo utawapeperusha; upepo wa kisulisuli utawatawanya; nawe utamfurahia BWANA, utajitukuza katika Mtakatifu wa Israeli.
Jua halitakuwa nuru yako tena wakati wa mchana, Wala mwezi hautakupa nuru kwa mwangaza wake; Bali BWANA atakuwa nuru ya milele kwako, Na Mungu wako atakuwa utukufu wako.
Nawe utakuwa taji la uzuri katika mkono wa BWANA, na kilemba cha kifalme mkononi mwa Mungu wako.
Nikatia kishaufu puani mwako, na herini masikioni mwako, na taji zuri juu ya kichwa chako.
Na wakuu wa Yuda watasema mioyoni mwao, Wenyeji wa Yerusalemu wana nguvu katika BWANA wa majeshi, Mungu wao.
Maana dhiki yetu nyepesi, iliyo ya muda mfupi tu, yatuandalia utukufu wa milele uzidio kuwa mwingi sana;