Basi sasa, angalia, BWANA ametia pepo wa uongo vinywani mwa manabii wako hawa; naye BWANA amenena mabaya juu yako.
Isaya 19:14 - Swahili Revised Union Version Yeye BWANA ametia roho ya ushupavu katika moyo wa Misri, nao wameikosesha Misri katika matendo yake yote, kama mlevi aendavyo huku na huko akitapika. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mwenyezi-Mungu amewamwagia hali ya vurugu, wakawapotosha Wamisri katika mipango yao yote, wakawa kama mlevi anayeyumbayumba akitapika. Biblia Habari Njema - BHND Mwenyezi-Mungu amewamwagia hali ya vurugu, wakawapotosha Wamisri katika mipango yao yote, wakawa kama mlevi anayeyumbayumba akitapika. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mwenyezi-Mungu amewamwagia hali ya vurugu, wakawapotosha Wamisri katika mipango yao yote, wakawa kama mlevi anayeyumbayumba akitapika. Neno: Bibilia Takatifu Mwenyezi Mungu amewamwagia roho ya kizunguzungu; wanaifanya Misri iyumbayumbe katika yale yote inayoyafanya, kama vile mlevi ayumbayumbavyo katika kutapika kwake. Neno: Maandiko Matakatifu bwana amewamwagia roho ya kizunguzungu; wanaifanya Misri iyumbayumbe katika yale yote inayoyafanya, kama vile mlevi ayumbayumbavyo katika kutapika kwake. BIBLIA KISWAHILI Yeye BWANA ametia roho ya ushupavu katika moyo wa Misri, nao wameikosesha Misri katika matendo yake yote, kama mlevi aendavyo huku na huko akitapika. |
Basi sasa, angalia, BWANA ametia pepo wa uongo vinywani mwa manabii wako hawa; naye BWANA amenena mabaya juu yako.
Nami nitawaamsha Wamisri juu ya Wamisri; nao watapigana, kila mtu na ndugu yake, na kila mtu na jirani yake, mji juu ya mji, na ufalme juu ya ufalme.
Dunia inalewalewa kama mlevi, nayo inawayawaya kama machela; na mzigo wa dhambi zake utailemea; nayo itaanguka, wala haitainuka tena.
kwa sababu hiyo mimi nitafanya tena kazi ya ajabu kati ya watu hawa, kazi ya ajabu na mwujiza; na akili za watu wao wenye akili zitapotea, na ufahamu wa wenye busara wao utafichwa.
Kuhusu watu wangu, watoto ndio wanaowaonea, na wanawake ndio wanaowatawala. Enyi watu wangu, wakuongozao wakukosesha, waiharibu njia ya mapito yako.
Kwa maana wawaongozao watu hawa ndio wawakoseshao, na hao walioongozwa na watu hao wameangamia.
Nawe utawaambia hivi, BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Nyweni, na kulewa, na kutapika, na kuanguka msiinuke tena, kwa sababu ya upanga nitakaoutuma kati yenu.
na Moabu atagaagaa katika matapiko yake, naye atadhihakiwa. Kwa maana Israeli, je! Hakuwa dhihaka kwako?
Yesu akajibu, akasema, Enyi kizazi kisichoamini, kilichopotoka, nitakaa pamoja nanyi hadi lini? Nitachukuliana nanyi hadi lini? Mleteni huku kwangu.
Kisha Mungu akatuma roho mbaya kati ya Abimeleki na watu wa Shekemu; nao watu wa Shekemu wakamtendea Abimeleki kwa udanganyifu;