Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Mathayo 17:17 - Swahili Revised Union Version

17 Yesu akajibu, akasema, Enyi kizazi kisichoamini, kilichopotoka, nitakaa pamoja nanyi hadi lini? Nitachukuliana nanyi hadi lini? Mleteni huku kwangu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

17 Yesu akajibu, “Enyi kizazi kisicho na imani, kilichopotoka! Nitakaa nanyi mpaka lini? Nitawavumilia nyinyi mpaka lini? Mleteni hapa huyo mtoto.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

17 Yesu akajibu, “Enyi kizazi kisicho na imani, kilichopotoka! Nitakaa nanyi mpaka lini? Nitawavumilia nyinyi mpaka lini? Mleteni hapa huyo mtoto.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

17 Yesu akajibu, “Enyi kizazi kisicho na imani, kilichopotoka! Nitakaa nanyi mpaka lini? Nitawavumilia nyinyi mpaka lini? Mleteni hapa huyo mtoto.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

17 Isa akajibu, “Enyi kizazi kisichoamini na kilichopotoka! Nitakaa nanyi hadi lini? Nitawavumilia hadi lini? Mleteni mvulana hapa kwangu.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

17 Isa akajibu, “Enyi kizazi kisichoamini na kilichopotoka! Nitakaa nanyi mpaka lini? Nitawavumilia mpaka lini? Mleteni mvulana hapa kwangu.”

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

17 Yesu akajibu, akasema, Enyi kizazi kisichoamini, kilichopotoka, nitakaa pamoja nanyi hadi lini? Nitachukuliana nanyi hadi lini? Mleteni huku kwangu.

Tazama sura Nakili




Mathayo 17:17
25 Marejeleo ya Msalaba  

Miaka arubaini nilichukizwa na kizazi kile, Nikasema, Hawa ni watu wenye mioyo inayopotoka, Na wanaopuuza njia zangu.


Basi Musa na Haruni wakaingia kwa Farao, na kumwambia, BWANA, Mungu wa Waebrania, asema hivi, Je! Utakataa hata lini kujinyenyekeza mbele zangu? Wape watu wangu ruhusa waende zao, ili wanitumikie.


BWANA akamwambia Musa, Mtakataa kuyashika maagizo yangu na sheria zangu hata lini?


Enyi wajinga, hata lini mtapenda ujinga? Na wenye dharau kupenda dharau yao, Na wapumbavu kuchukia maarifa?


Ewe mvivu, utalala hadi lini? Utaondoka lini katika usingizi wako?


Yeye BWANA ametia roho ya ushupavu katika moyo wa Misri, nao wameikosesha Misri katika matendo yake yote, kama mlevi aendavyo huku na huko akitapika.


Ee Yerusalemu, jioshe moyo wako usiwe na uovu, upate kuokoka. Mawazo yako mabaya yatakaa ndani yako hata lini?


BWANA akamwuliza Musa, Je! Watu hawa watanidharau hadi lini? Wasiniamini hadi lini? Nijapokuwa nimefanya ishara hizo zote kati yao.


Je! Nivumilie na mkutano mwovu huu uninung'unikiao hadi lini? Nimesikia manung'uniko ya wana wa Israeli, waninung'unikiayo.


Wala hakufanya miujiza mingi huko, kwa sababu ya kutoamini kwao.


Naye Yesu akafahamu, akawaambia, Mbona mnabishana ninyi kwa ninyi, enyi wa imani haba, kwa sababu hamna mikate?


Nilimleta kwa wanafunzi wako, wasiweze kumponya.


Yesu akamkemea pepo, naye akamtoka; yule mvulana akapona tangu saa ile.


Basi, ikiwa Mungu huyavika hivi majani ya kondeni, yaliyopo leo, na kesho hutupwa katika tanuri, je! Hatazidi sana kuwavika ninyi, enyi wa imani haba?


Akawaambia, Mbona mmekuwa waoga, enyi wa imani haba? Mara akaondoka, akazikemea pepo na bahari; kukawa shwari kuu.


Baadaye akaonekana na wale kumi na mmoja walipokuwa wakila, akawakemea kwa kutoamini kwao na ugumu wa mioyo yao, kwa kuwa hawakuwasadiki wale waliomwona alipofufuka katika wafu.


Akawajibu, akasema, Enyi kizazi kisichoamini, nikae nanyi hadi lini? Nichukuliane nanyi hadi lini? Mleteni kwangu.


Akawaambia, Enyi msiofahamu, wenye mioyo mizito ya kuamini yote waliyoyasema manabii!


Yesu akajibu akasema, Enyi kizazi kisicho na imani, kilichopotoka, nitakaa nanyi na kuwachukulia hata lini? Mlete mwanao hapa.


Kisha akamwambia Tomaso, Lete hapa kidole chako; uitazame mikono yangu; ulete na mkono wako uutie ubavuni mwangu, wala usiwe asiyeamini, bali aaminiye.


Na kwa muda wa miaka kama arubaini akawavumilia katika jangwa.


Akawashuhudia kwa maneno mengine mengi sana na kuwaonya, akisema, Jiokoeni na kizazi hiki chenye ukaidi.


Laiti mngechukuliana nami katika upumbavu wangu kidogo! Naam, mchukuliane nami.


Wametenda mambo ya uharibifu, Hawawi watoto wake, hii ndiyo ila yao; Wao ni kizazi chenye ukaidi, kilichopotoka.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo