Isaya 1:2 - Swahili Revised Union Version Sikieni, enyi mbingu, tega sikio, Ee nchi, kwa maana BWANA amenena; Nimewalisha watoto na kuwalea, nao wameniasi. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Sikilizeni enyi mbingu, tega sikio ee dunia. Mimi nimewalea wanangu wakakua, lakini sasa wameniasi! Biblia Habari Njema - BHND Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Sikilizeni enyi mbingu, tega sikio ee dunia. Mimi nimewalea wanangu wakakua, lakini sasa wameniasi! Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Sikilizeni enyi mbingu, tega sikio ee dunia. Mimi nimewalea wanangu wakakua, lakini sasa wameniasi! Neno: Bibilia Takatifu Sikieni, enyi mbingu! Sikilizeni, enyi dunia! Kwa maana Mwenyezi Mungu amesema: “Nimewalisha watoto na kuwalea, lakini wameniasi mimi. Neno: Maandiko Matakatifu Sikieni, enyi mbingu! Sikilizeni, enyi dunia! Kwa maana bwana amesema: “Nimewalisha watoto na kuwalea, lakini wameniasi mimi. BIBLIA KISWAHILI Sikieni, enyi mbingu, tega sikio, Ee nchi, kwa maana BWANA amenena; Nimewalisha watoto na kuwalea, nao wameniasi. |
Ole wa watoto waasi; asema BWANA; watakao mashauri lakini hawayataki kwangu mimi; wajifunikao kifuniko lakini si cha roho yangu; wapate kuongeza dhambi juu ya dhambi;
Kwa maana watu hawa ni watu waasi, watoto wasemao uongo, watoto wasiotaka kuisikia sheria ya BWANA;
Karibuni, enyi mataifa, mpate kusikia; sikilizeni, enyi makabila ya watu; dunia na isikie, na chote kiijazacho, ulimwengu na vitu vyote viutokavyo.
Maana wewe ndiwe Baba yetu, ijapokuwa Abrahamu hatujui, wala Israeli hatukiri; wewe, BWANA, ndiwe Baba yetu, mkombozi wetu tangu milele ndilo jina lako.
Nitazameni, nitazameni. Mchana kutwa nimewanyoshea mikono yangu watu walioasi, watu waendao katika njia isiyo njema, wakifuata mawazo yao wenyewe;
Rudini, enyi watoto waasi, mimi nitaponya maasi yenu. Tazama, tumekuja kwako; maana wewe u BWANA, Mungu wetu.
Watakuja kwa kulia, na kwa maombi nitawaongoza; nitawapitisha kwenye mito ya maji, katika njia iliyonyoka; katika njia hiyo hawatajikwaa; maana mimi ni baba wa Israeli, na Efraimu ni mzaliwa wa kwanza wangu.
Sikia, Ee nchi; tazama, nitaleta mabaya juu ya watu hawa, naam, matunda ya mawazo yao, kwa sababu hawakuyasikiliza maneno yangu; tena kwa habari ya sheria yangu, wameikataa.
Ukawatungie mithali nyumba ya kuasi, ukawaambie, Bwana MUNGU asema hivi; Teleka sufuria, liteleke; ukatie maji ndani yake;
kwa sababu hiyo, enyi milima ya Israeli, lisikieni neno la Bwana MUNGU; Bwana MUNGU aiambia hivi hiyo milima na vilima, mito ya maji na mabonde, mahali palipoharibika na kuwa ukiwa, na miji iliyoachwa na watu, ambayo imekuwa mateka, na kuzomewa na mabaki ya mataifa, walio karibu pande zote;
Lisikieni neno hili alilolisema BWANA juu yenu, enyi wana wa Israeli, juu ya jamaa yote niliowapandisha kutoka nchi ya Misri, nikisema,
Hili ndilo neno la BWANA lililomjia Mika, Mmoreshathi, katika siku za Yothamu, na Ahazi, na Hezekia, wafalme wa Yuda; maono aliyoyaona kuhusu Samaria na Yerusalemu.
Sikilizeni, enyi watu wa kabila zote; sikiliza, Ee dunia, na vyote vilivyomo; Bwana MUNGU na ashuhudie juu yenu, yeye Bwana kutoka hekalu lake takatifu.
Bali mimi, hakika nimejaa nguvu kwa Roho ya BWANA; nimejaa hukumu na uwezo; nimhubirie Yakobo kosa lake, na Israeli dhambi yake.
Mwana humheshimu baba yake, na mtumishi humcha bwana wake; basi, kama mimi ni baba yenu, heshima yangu iko wapi? Na kama mimi ni bwana wenu, kicho changu ki wapi? BWANA wa majeshi awauliza ninyi, enyi makuhani, mnaolidharau jina langu. Nanyi mwasema, Tumelidharau jina lako kwa jinsi gani?
na huko jangwani, ulipoona alivyokuchukua BWANA, Mungu wako, kama mtu amchukuavyo mwanawe, njia yote mliyoiendea, hata mkafika mahali hapa.
Nazishuhudiza mbingu na nchi juu yenu hivi leo, kuwa nimekuwekea mbele yako uzima na mauti, baraka na laana; basi chagua uzima, ili uwe hai, wewe na uzao wako;
naziita mbingu na nchi hivi leo kushuhudia, kwamba karibu mtaangamia kabisa juu ya nchi mwivukiayo Yordani kuimiliki, hamtafanya siku zenu ziwe nyingi juu yake, ila mtaangamizwa kabisa.