Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Isaya 34:1 - Swahili Revised Union Version

1 Karibuni, enyi mataifa, mpate kusikia; sikilizeni, enyi makabila ya watu; dunia na isikie, na chote kiijazacho, ulimwengu na vitu vyote viutokavyo.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

1 Karibieni mkasikilize enyi mataifa, tegeni sikio enyi watu. Sikiliza ee dunia na vyote vilivyomo, ulimwengu na vyote vitokavyo humo!

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

1 Karibieni mkasikilize enyi mataifa, tegeni sikio enyi watu. Sikiliza ee dunia na vyote vilivyomo, ulimwengu na vyote vitokavyo humo!

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

1 Karibieni mkasikilize enyi mataifa, tegeni sikio enyi watu. Sikiliza ee dunia na vyote vilivyomo, ulimwengu na vyote vitokavyo humo!

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

1 Njooni karibu, enyi mataifa, nanyi msikilize; sikilizeni kwa makini, enyi makabila ya watu! Dunia na isikie, navyo vyote vilivyo ndani yake, ulimwengu na vyote vinavyotoka ndani yake!

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

1 Njooni karibu, enyi mataifa, nanyi msikilize; sikilizeni kwa makini, enyi kabila za watu! Dunia na isikie, navyo vyote vilivyo ndani yake, ulimwengu na vyote vitokavyo ndani yake!

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

1 Karibuni, enyi mataifa, mpate kusikia; sikilizeni, enyi makabila ya watu; dunia na isikie, na chote kiijazacho, ulimwengu na vitu vyote viutokavyo.

Tazama sura Nakili




Isaya 34:1
25 Marejeleo ya Msalaba  

Mungu akamwambia Nuhu, Mwisho wa kila kiumbe umefika mbele zangu; kwa sababu wameijaza dunia maovu, basi nitawaangamiza pamoja na dunia.


Nchi na vyote vilivyomo ni mali ya BWANA, Dunia na wote wakaao ndani yake.


Mungu, Mungu BWANA, amenena, ameiita nchi, Toka maawio ya jua hadi machweo yake.


Semeni katika mataifa, BWANA ametamalaki; Naam, ulimwengu umethibitika usitikisike, Atawahukumu watu kwa adili.


Sikieni, enyi mbingu, tega sikio, Ee nchi, kwa maana BWANA amenena; Nimewalisha watoto na kuwalea, nao wameniasi.


Enyi watu mkaao katika ulimwengu wote, na wenyeji wa dunia, bendera ikiinuliwa milimani, angalieni; na wakipiga tarumbeta, sikieni.


Sikieni, ninyi mlio mbali, niliyoyatenda; na ninyi mlio karibu, kirini uwezo wangu.


Nyamazeni mbele zangu, enyi visiwa, na mataifa wajipatie nguvu mpya; na waje karibu wakanene; na tukaribiane pamoja kwa hukumu.


Na wakusanyike mataifa yote, kabila zote wakutanike; ni nani miongoni mwao awezaye kuhubiri neno hili, na kutuonesha mambo ya zamani? Na walete mashahidi wao, wapate kuhesabiwa kuwa na haki; au na wasikie, wakaseme, Ni kweli.


Nikaribieni, sikieni haya; tokea mwanzo sikunena kwa siri; tangu yalipokuwapo, mimi nipo; na sasa Bwana MUNGU amenituma, na roho yake.


Nisikilizeni, enyi visiwa; tegeni masikio yenu, enyi makabila ya watu mlio mbali sana; BWANA ameniita tangu tumboni; toka tumbo la mama yangu amenitaja jina langu.


Ni nani huyu atokaye Edomu, Atokaye Bosra akiwa na mavazi yenye madoa mekundu? Huyu aliye na nguo za fahari, Anayekwenda katika ukuu wa uweza wake? Ndimi nisemaye kwa haki, Niliye hodari wa kuokoa.


Ee nchi, nchi, nchi, lisikie neno la BWANA.


Kuhusu Edomu. BWANA wa majeshi asema hivi, Je! Hakuna tena hekima katika Temani? Mashauri yamewapotea wenye busara? Je! Imetoweka hekima yao?


Bwana MUNGU asema hivi; Je! Wewe ndiwe niliyemnena zamani za kale, kwa vinywa vya watumishi wangu, manabii wa Israeli, waliotabiri siku zile kwa muda wa miaka mingi, ya kwamba nitakuleta upigane nao?


Maono yake Obadia. Ndivyo asemavyo Bwana MUNGU juu ya Edomu; Tumepata habari kwa BWANA, Na mjumbe ametumwa kati ya mataifa, Akisema, Haya, inukeni ninyi; Na tuinuke tupigane naye.


maana, Dunia ni mali ya Bwana na vyote viijazavyo.


Sikilizeni, enyi mbingu, nami nitanena; Na nchi isikie maneno ya kinywa changu.


naziita mbingu na nchi hivi leo kushuhudia, kwamba karibu mtaangamia kabisa juu ya nchi mwivukiayo Yordani kuimiliki, hamtafanya siku zenu ziwe nyingi juu yake, ila mtaangamizwa kabisa.


Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho anayaambia makanisa. Yeye ashindaye, nitampa kula matunda ya mti wa uzima, ulio katika bustani ya Mungu.


Sikieni, enyi wafalme; tegeni masikio, enyi wakuu; Mimi, naam mimi, nitamwimbia BWANA; Nitamhimidi BWANA, Mungu wa Israeli.


Na waangamie vivyo hivyo adui zako wote, Ee BWANA. Bali wao wampendao na wawe kama jua hapo litokapo kwa nguvu zake. Nayo nchi ikastarehe miaka arubaini.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo