Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Mika 3:8 - Swahili Revised Union Version

8 Bali mimi, hakika nimejaa nguvu kwa Roho ya BWANA; nimejaa hukumu na uwezo; nimhubirie Yakobo kosa lake, na Israeli dhambi yake.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

8 Lakini kwa upande wangu, nimejazwa nguvu na roho ya Mwenyezi-Mungu; nimejaliwa kujua haki na kuwa na uwezo niwatangazie wazawa wa Yakobo kosa lao, niwaambie Waisraeli dhambi yao.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

8 Lakini kwa upande wangu, nimejazwa nguvu na roho ya Mwenyezi-Mungu; nimejaliwa kujua haki na kuwa na uwezo niwatangazie wazawa wa Yakobo kosa lao, niwaambie Waisraeli dhambi yao.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

8 Lakini kwa upande wangu, nimejazwa nguvu na roho ya Mwenyezi-Mungu; nimejaliwa kujua haki na kuwa na uwezo niwatangazie wazawa wa Yakobo kosa lao, niwaambie Waisraeli dhambi yao.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

8 Lakini mimi nimejazwa nguvu, nimejazwa Roho wa Mwenyezi Mungu, haki na uweza, kumtangazia Yakobo kosa lake, na Israeli dhambi yake.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

8 Lakini kuhusu mimi, nimejazwa nguvu, nimejazwa Roho wa bwana, haki na uweza, kumtangazia Yakobo kosa lake, na Israeli dhambi yake.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

8 Bali mimi, hakika nimejaa nguvu kwa Roho ya BWANA; nimejaa hukumu na uwezo; nimhubirie Yakobo kosa lake, na Israeli dhambi yake.

Tazama sura Nakili




Mika 3:8
28 Marejeleo ya Msalaba  

Kwa kuwa nimejaa maneno; Roho iliyo ndani yangu hunihimiza.


Piga kelele, usiache, Paza sauti yako kama tarumbeta; Uwahubirie watu wangu kosa lao, Na nyumba ya Yakobo dhambi zao.


Roho ya Bwana MUNGU i juu yangu; kwa sababu BWANA amenitia mafuta niwahubirie wanyenyekevu habari njema; amenituma ili kuwatibu waliovunjika moyo, kuwatangazia mateka uhuru wao, na hao waliofungwa habari za kufunguliwa kwao.


Kutangaza mwaka wa BWANA uliokubaliwa, na siku ya kisasi cha Mungu wetu; kuwafariji wote waliao;


Maana, tazama, nimekufanya leo kuwa mji wenye boma, na nguzo ya chuma, na kuta za shaba, juu ya nchi yote; juu ya wafalme wa Yuda, na juu ya wakuu wake, na juu ya makuhani wake, na juu ya watu wa nchi hii.


Nami nikisema, Sitamtaja, wala sitasema tena kwa jina lake; basi, ndipo moyoni mwangu kumekuwamo kama moto uwakao, uliofungwa ndani ya mifupa yangu, nami nimechoka kwa kustahimili, wala siwezi kujizuia.


Lakini nimejaa ghadhabu ya BWANA; nimechoka kwa kujizuia; imwageni juu ya watoto walio njiani, na juu ya kusanyiko la vijana pia; maana hata mume atatwaliwa pamoja na mkewe, mzee pamoja na yeye aliyetimiza siku zake.


Manabii wako wameona maono kwa ajili yako Ya ubatili na upumbavu Wala hawakufunua uovu wako, Wapate kurudisha kufungwa kwako; Bali wameona mabashiri ya ubatili kwa ajili yako Na sababu za kuhamishwa.


Mwanadamu, uujulishe Yerusalemu machukizo yake,


Je! Utawahukumu, mwanadamu, utawahukumu? Uwajulishe machukizo ya baba zao;


Na wewe, mwanadamu, je! Utauhukumu, utauhukumu mji huu wa damu? Basi uujulishe machukizo yake yote.


Tena BWANA akaniambia, Mwanadamu, utawahukumu Ohola na Oholiba? Basi watangazie matendo yao maovu.


Basi roho ikaniinua, ikanichukua mahali pengine; nami nikaenda kwa uchungu, na hasira kali rohoni mwangu, na mkono wa BWANA ulikuwa juu yangu kwa nguvu.


Na wewe, mwanadamu, waoneshe wana wa Israeli nyumba hii, ili wayatahayarikie maovu yao; na waipime hesabu yake.


kwa maana alikuwa akiwafundisha kama mtu mwenye mamlaka, wala si kama waandishi wao.


na Yakobo, mwana wa Zebedayo, na Yohana nduguye Yakobo, akawapa jina la Boanerge, maana yake, wana wa ngurumo;


Na neno langu na kuhubiri kwangu hakukuwa kwa maneno ya hekima yenye kushawishi akili za watu, bali kwa dalili za Roho na za nguvu,


Tufuate:

Matangazo


Matangazo