Hosea 7:16 - Swahili Revised Union Version Wao hurudi, lakini si kwake Aliye Juu; wamekuwa kama upinde usiotumainika; wakuu wao wataanguka kwa upanga, kwa sababu ya ujeuri wa ndimi zao; na kwa sababu hiyo watachekwa katika nchi ya Misri. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Wanaigeukia miungu batili, wako kama uta uliolegea. Viongozi wao watakufa kwa upanga, kwa sababu ya maneno yao ya kiburi. Kwa hiyo, watadharauliwa nchini Misri. Biblia Habari Njema - BHND Wanaigeukia miungu batili, wako kama uta uliolegea. Viongozi wao watakufa kwa upanga, kwa sababu ya maneno yao ya kiburi. Kwa hiyo, watadharauliwa nchini Misri. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Wanaigeukia miungu batili, wako kama uta uliolegea. Viongozi wao watakufa kwa upanga, kwa sababu ya maneno yao ya kiburi. Kwa hiyo, watadharauliwa nchini Misri. Neno: Bibilia Takatifu Hawamgeukii Yeye Aliye Juu Sana, wako kama upinde wenye kasoro. Viongozi wao wataanguka kwa upanga kwa sababu ya maneno yao ya jeuri. Kwa ajili ya hili watadhihakiwa katika nchi ya Misri. Neno: Maandiko Matakatifu Hawamgeukii Yeye Aliye Juu Sana, wako kama upinde wenye kasoro. Viongozi wao wataanguka kwa upanga kwa sababu ya maneno yao ya jeuri. Kwa ajili ya hili watadhihakiwa katika nchi ya Misri. BIBLIA KISWAHILI Wao hurudi, lakini si kwake Aliye Juu; wamekuwa kama upinde usiotumainika; wakuu wao wataanguka kwa upanga, kwa sababu ya ujeuri wa ndimi zao; na kwa sababu hiyo watachekwa katika nchi ya Misri. |
Waliosema, Kwa ndimi zetu tutashinda; Midomo yetu ni yetu wenyewe, Ni nani aliye bwana juu yetu?
Kwa ajili ya kuonewa kwao wanyonge, Kwa ajili ya kuugua kwao wahitaji, Sasa nitasimama, asema BWANA, Nitamweka salama yeye wanayemfyonya.
Nafsi yangu i kati ya simba, Nitastarehe kati yao waliowaka moto. Wanadamu meno yao ni mikuki na mishale, Na ndimi zao ni upanga mkali.
Kwa maana Yerusalemu umebomolewa na Yuda wameanguka, kwa sababu ulimi wao na matendo yao ni kinyume cha BWANA, hata wakayachukiza macho ya utukufu wake.
Hapo ndipo waliposema, Njooni na tufanye mashauri juu ya Yeremia; maana sheria haitampotea kuhani, wala shauri halitampotea mwenye hekima, wala neno halitampotea nabii. Njooni, na tumpige kwa ndimi zetu, wala tusiyaangalie maneno yake yoyote.
Na pamoja na hayo yote dada yake, Yuda mwenye hiana, hajanirudia mimi kwa moyo wake wote, bali kwa unafiki, asema BWANA.
Maana BWANA wa majeshi Mungu wa Israeli, asema hivi, Kama hasira yangu, na ghadhabu yangu, ilivyomwagwa juu ya hao wakaao Yerusalemu, ndivyo ghadhabu yangu itakavyomwagwa juu yenu, mtakapoingia Misri; nanyi mtakuwa apizo, na ajabu, na laana, na aibu; wala hamtapaona mahali hapa tena.
Bwana MUNGU asema hivi; Utakinywea kikombe cha dada yako; chenye kina kirefu na kipana; utadhihakiwa na kudharauliwa; nacho kimejaa sana.
Nao walipoyafikia mataifa yale waliyoyaendea, walilitia unajisi jina langu takatifu; kwa kuwa watu waliwanena, wakisema, Watu hawa ni watu wa BWANA, nao wametoka katika nchi yake.
Naye atanena maneno kinyume chake Aliye Juu, naye atawadhoofisha watakatifu wake Aliye Juu; naye ataazimu kubadili majira na sheria; nao watatiwa mikononi mwake kwa nyakati tatu na nusu
Hatarudi tena nchi ya Misri; bali huyo Mwashuri atakuwa mfalme wake; kwa sababu walikataa kurejea.
Na watu wangu wamejipinda kuniacha; ingawa wawaita kwenda kwake Aliye Juu, hapana hata mmoja atakayemtukuza.
Ee Efraimu, nikutendee nini? Ee Yuda, nikutendee nini? Kwa maana fadhili zenu ni kama wingu la asubuhi na kama umande utowekao mapema.
Ole wao! Kwa kuwa wamenikimbia; uharibifu na uwapate! Kwa kuwa wameniasi; ingawa ninataka kuwakomboa, hata hivyo wamenena uongo juu yangu.
Hawatakaa katika nchi ya BWANA; lakini Efraimu atarudi Misri, nao watakula chakula najisi katika Ashuru.
Hawatammiminia BWANA divai, wala hazitampendeza sadaka zao; mkate wao utakuwa kama chakula cha matanga kwao; wote watakaokila watatiwa unajisi; kwa maana mkate wao utakuwa kwa shauku zao; hautaingia katika nyumba ya BWANA.
Kwa maana, tazama, wamekwenda zao ili kukimbia uharibifu, lakini Misri itawakusanya, Nofu itawazika; vitu vyao vya fedha viwapendezavyo, magugu yatavimiliki; miiba itakuwa katika hema zao.
Maneno yenu yamekuwa magumu juu yangu, asema BWANA. Lakini ninyi mwasema, Tumesema maneno juu yako kwa namna gani?
Mmesema, Kumtumikia Mungu hakuna faida; na, Tumepata faida gani kwa kuyashika maagizo yake, na kwa kwenda kwa huzuni mbele za BWANA wa majeshi?
Basi, nawaambia, Kila neno lisilo maana, watakalolinena wanadamu, watatoa hesabu ya neno hilo siku ya hukumu.
Na wale penye mwamba ndio wale ambao wasikiapo hulipokea lile neno kwa furaha; nao hawana mizizi, huamini kitambo kidogo, na wakati wa kujaribiwa hujitenga.
Vivyo hivyo ulimi nao ni kiungo kidogo, nao hujivunia matendo makuu. Angalieni jinsi moto mdogo uwashavyo msitu mkubwa sana.
maana mtu huyu mwenye haki akikaa kati yao, kwa kuona na kusikia, alijitesa roho yake yenye haki, siku baada ya siku, kwa matendo yao yasiyo na sheria;
Naye akapewa kinywa cha kunena maneno makuu, ya kukufuru. Akapewa uwezo wa kufanya kazi yake miezi arubaini na miwili.