Danieli 7:25 - Swahili Revised Union Version25 Naye atanena maneno kinyume chake Aliye Juu, naye atawadhoofisha watakatifu wake Aliye Juu; naye ataazimu kubadili majira na sheria; nao watatiwa mikononi mwake kwa nyakati tatu na nusu Tazama suraMatoleo zaidiBiblia Habari Njema25 Huyo atamkufuru Mungu Mkuu na kuwatesa watakatifu wake. Atajaribu kubadilisha nyakati na sheria zao, na watakatifu watatiwa mikononi mwake kwa muda wa miaka mitatu na nusu. Tazama suraBiblia Habari Njema - BHND25 Huyo atamkufuru Mungu Mkuu na kuwatesa watakatifu wake. Atajaribu kubadilisha nyakati na sheria zao, na watakatifu watatiwa mikononi mwake kwa muda wa miaka mitatu na nusu. Tazama suraBiblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza25 Huyo atamkufuru Mungu Mkuu na kuwatesa watakatifu wake. Atajaribu kubadilisha nyakati na sheria zao, na watakatifu watatiwa mikononi mwake kwa muda wa miaka mitatu na nusu. Tazama suraNeno: Bibilia Takatifu25 Atanena maneno kinyume cha Yeye Aliye Juu Sana na kuwatesa watakatifu wake, huku akijaribu kubadili majira na sheria. Watakatifu watatiwa chini ya mamlaka yake kwa wakati, nyakati mbili, na nusu wakati. Tazama suraNeno: Maandiko Matakatifu25 Atanena maneno kinyume cha Yeye Aliye Juu Sana na kuwaonea watakatifu wake, huku akijaribu kubadili majira na sheria. Watakatifu watatiwa chini ya mamlaka yake kwa wakati, nyakati mbili, na nusu wakati. Tazama suraSwahili Roehl Bible 193725 Tena atasema maneno ya kumbeza Alioko huko juu, nao watakatifu wake Alioko huko juu atawapondaponda; tena atajipa moyo wa kuzigauza sikukuu, atoe nyingine, hata maongozi, atoe mengine. Nao watakatifu watatiwa mikononi mwake kipande cha siku na vipande viwili vya siku na nusu ya kipande cha siku. Tazama sura |
Nami nikamsikia yule mtu aliyevikwa nguo za kitani, aliyekuwa juu ya maji ya mto, hapo alipoinua mkono wake wa kulia na mkono wake wa kushoto kuelekea mbinguni; akaapa kwa yeye aliye hai milele na milele, ya kwamba itakuwa nyakati tatu na nusu; tena watakapokuwa wamekwisha kuvunja nguvu za hao watu watakatifu, ndipo mambo hayo yote yatakapotimizwa.
ya kuwa utafukuzwa mbali na wanadamu, na makao yako yatakuwa pamoja na wanyama wa mwituni, nawe utalazimishwa kula majani kama ng'ombe, nawe utanyeshewa na umande wa mbinguni, na nyakati saba zitapita juu yako; hata utakapojua ya kuwa Aliye Juu ndiye anayemiliki katika ufalme wa wanadamu, naye humpa yeye amtakaye, awaye yote.