Hosea 6:2 - Swahili Revised Union Version Baada ya siku mbili atatufufua; siku ya tatu atatuinua, nasi tutaishi mbele zake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Baada ya siku mbili, atatupa uhai tena, naam, siku ya tatu atatufufua ili tuweze kuishi pamoja naye. Biblia Habari Njema - BHND Baada ya siku mbili, atatupa uhai tena, naam, siku ya tatu atatufufua ili tuweze kuishi pamoja naye. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Baada ya siku mbili, atatupa uhai tena, naam, siku ya tatu atatufufua ili tuweze kuishi pamoja naye. Neno: Bibilia Takatifu Baada ya siku mbili atatufufua; katika siku ya tatu atatuinua, ili tuweze kuishi mbele zake. Neno: Maandiko Matakatifu Baada ya siku mbili atatufufua; katika siku ya tatu atatuinua, ili tuweze kuishi mbele zake. BIBLIA KISWAHILI Baada ya siku mbili atatufufua; siku ya tatu atatuinua, nasi tutaishi mbele zake. |
Rudi, ukamwambie Hezekia, mkuu wa watu wangu, BWANA, Mungu wa Daudi baba yako asema hivi, Nimeyasikia maombi yako, na kuyaona machozi yako; tazama, nitakuponya; siku ya tatu utapanda nyumbani kwa BWANA.
Wewe, uliyetuonesha mateso mengi, mabaya, Utatuhuisha tena. Utatupandisha juu tena Kutoka katika vina virefu chini ya nchi.
Wafu wako wataishi, maiti zangu zitafufuka; amkeni, kaimbeni, ninyi mnaokaa mavumbini, kwa maana umande wako ni kama umande wa mimea, nayo ardhi itawatoa waliokufa.
Na tena nuru ya mwezi itakuwa kama nuru ya jua, na nuru ya jua itaongezeka mara saba, kama nuru ya siku saba, katika siku ile BWANA atakapofunga mapigo ya watu wake, na kuliponya pigo la jeraha lao.
Nitawakomboa kwa nguvu za kaburi; nitawaokoa kutoka kwa mauti; ewe mauti, ya wapi mapigo yako? Ewe kaburi, ku wapi kuharibu kwako? Huruma itafichika machoni mwangu.
Wala hawafikiri mioyoni mwao ya kwamba naukumbuka uovu wao wote; sasa matendo yao wenyewe yamewazunguka pande zote; yako mbele za uso wangu.
Bado kitambo kidogo na ulimwengu haunioni tena; bali ninyi mnaniona. Na kwa sababu mimi ni hai, ninyi nanyi mtakuwa hai.
Kwa maana kama tukiishi, twaishi kwa Bwana, au kama tukifa, twafa kwa Bwana. Basi kama tukiishi au kama tukifa, tu mali ya Bwana.