Uniponye, unitoe, Katika mkono wa wageni. Vinywa vyao vyasema visivyofaa, Na mkono wao wa kulia ni mkono wa uongo.
Hosea 5:7 - Swahili Revised Union Version Wamemtendea BWANA kwa hila; maana wamezaa wana wageni; sasa mwezi huu uandamao utawaangamiza pamoja na mashamba yao. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Wamevunja uaminifu kwa Mwenyezi-Mungu, wamezaa watoto walio haramu. Mwezi mwandamo utawaangamiza, pamoja na mashamba yao. Biblia Habari Njema - BHND Wamevunja uaminifu kwa Mwenyezi-Mungu, wamezaa watoto walio haramu. Mwezi mwandamo utawaangamiza, pamoja na mashamba yao. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Wamevunja uaminifu kwa Mwenyezi-Mungu, wamezaa watoto walio haramu. Mwezi mwandamo utawaangamiza, pamoja na mashamba yao. Neno: Bibilia Takatifu Wao si waaminifu kwa Mwenyezi Mungu; wamezaa watoto haramu. Sasa sikukuu zao za Mwandamo wa Mwezi zitawaangamiza wao pamoja na mashamba yao. Neno: Maandiko Matakatifu Wao si waaminifu kwa bwana; wamezaa watoto haramu. Sasa sikukuu zao za Mwandamo wa Mwezi zitawaangamiza wao pamoja na mashamba yao. BIBLIA KISWAHILI Wamemtendea BWANA kwa hila; maana wamezaa wana wageni; sasa mwezi huu uandamao utawaangamiza pamoja na mashamba yao. |
Uniponye, unitoe, Katika mkono wa wageni. Vinywa vyao vyasema visivyofaa, Na mkono wao wa kulia ni mkono wa uongo.
Uinyoshe mikono yako toka juu, uniponye, Unitoe katika maji mengi, kutoka kwa mkono wa wageni,
Sikukuu zenu za mwezi mpya na karamu zenu zilizoamriwa, nafsi yangu yazichukia; mambo hayo yanilemea; nimechoka kuyachukua.
Naam, hukusikia; naam, hukujua; naam, tokea zamani sikio lako halikuzibuka; maana nilijua ya kuwa wewe watenda kwa hila nyingi, nawe umeitwa mkosaji tangu kuzaliwa kwako;
katika kukosa na kumkana BWANA, na katika kugeuka tusimfuate Mungu wetu, tukinena udhalimu na uasi, na kukusudia maneno ya uongo na kuyatoa moyoni.
Bali, kama vile mke amwachavyo mumewe kwa hiana, ndivyo mlivyonitenda mimi kwa hiana, Ee nyumba ya Israeli, asema BWANA.
Basi uwaambie, Bwana MUNGU asema hivi; Maneno yangu hayatakawilishwa tena hata moja, bali neno nitakalolinena litatimizwa, asema Bwana MUNGU.
Tena nitaikomesha furaha yake yote, na sikukuu zake, na siku zake za mwandamo wa mwezi, na sabato zake, na makusanyiko yake yote yaliyoamriwa.
Ole wao! Kwa kuwa wamenikimbia; uharibifu na uwapate! Kwa kuwa wameniasi; ingawa ninataka kuwakomboa, hata hivyo wamenena uongo juu yangu.
Nami nikawakatilia mbali wachungaji watatu katika mwezi mmoja; maana nafsi yangu ilikuwa imechoka kwa ajili yao, na nafsi zao pia walinichukia.