Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Hosea 5:8 - Swahili Revised Union Version

8 Pigeni tarumbeta katika Gibea, na baragumu katika Rama; pazeni sauti ya hofu katika Beth-aveni; nyuma yako, Ee Benyamini!

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

8 “Pigeni baragumu huko Gibea, na tarumbeta huko Rama. Pigeni king'ora huko Beth-aveni. Enyi watu wa Benyamini, adui yenu yuko nyuma!

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

8 “Pigeni baragumu huko Gibea, na tarumbeta huko Rama. Pigeni king'ora huko Beth-aveni. Enyi watu wa Benyamini, adui yenu yuko nyuma!

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

8 “Pigeni baragumu huko Gibea, na tarumbeta huko Rama. Pigeni king'ora huko Beth-aveni. Enyi watu wa Benyamini, adui yenu yuko nyuma!

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

8 “Pigeni tarumbeta huko Gibea, na baragumu huko Rama. Pazeni kelele za vita huko Beth-Aveni; ongoza, ee Benyamini.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

8 “Pigeni tarumbeta huko Gibea, baragumu huko Rama. Paza kilio cha vita huko Beth-Aveni, ongoza, ee Benyamini.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

8 Pigeni tarumbeta katika Gibea, na baragumu katika Rama; pazeni sauti ya hofu katika Beth-aveni; nyuma yako, Ee Benyamini!

Tazama sura Nakili




Hosea 5:8
20 Marejeleo ya Msalaba  

basi, na tutolewe watu saba katika wanawe, nasi tutawatundika mbele za BWANA katika Gibeoni, katika mlima wa BWANA. Mfalme akasema, Nitawatoa.


Akamweka mmoja katika Betheli, na wa pili akamweka katika Dani.


wamevuka kivuko; wamekwenda kulala katika Geba; Rama unatetemeka; Gibea wa Sauli umekimbia.


Tangazeni katika Yuda, hubirini katika Yerusalemu, na kusema, Pigeni baragumu katika nchi, pigeni kelele sana, na kusema, Jikusanyeni pamoja, tukaingie katika miji yenye boma.


Kimbieni mpate kuwa salama, enyi wana wa Benyamini; tokeni katika Yerusalemu, pigeni tarumbeta katika Tekoa, simamisheni ishara juu ya Beth-hakeremu; kwa maana mabaya yanachungulia toka kaskazini, na uharibifu mkuu.


Wakaao Samaria wataona hofu kwa ajili ya ndama za Beth-aveni; kwa maana watu wa mji huo wataulilia, na makuhani wake walioufurahia, kwa sababu ya utukufu wake; kwa maana umetoweka.


Ingawa wewe, Israeli, unafanya uzinzi, lakini asiasi Yuda; nanyi msiende Gilgali wala msipande mpaka Beth-aveni, wala msiape mkisema, Aishivyo BWANA.


Tia baragumu kinywani mwako. Kama tai, anakuja juu ya nyumba ya BWANA; kwa sababu wamelivunja agano langu, wameiasi sheria yangu.


Wamejiharibu mno, kama katika siku za Gibea; ataukumbuka uovu wao, atazilipiza dhambi zao.


Pigeni tarumbeta katika Sayuni, Pigeni na kelele katika mlima wangu mtakatifu; Wenyeji wote wa nchi na watetemeke; Kwa maana siku ya BWANA inakuja. Kwa sababu inakaribia;


Pigeni tarumbeta katika Sayuni, Takaseni saumu, kusanyeni kusanyiko kuu;


Je! Tarumbeta itapigwa mjini, watu wasiogope? Mji utapatikana na hali mbaya, asiyoileta BWANA?


Kisha Yoshua akatuma watu kutoka Yeriko mpaka mji wa Ai, ulio karibu na Beth-aveni, upande wa mashariki wa Betheli, akawaambia, akisema, Pandeni juu mkaipeleleze nchi, basi wakapanda juu wakaupeleleza Ai.


Kutoka Efraimu waliteremka wao ambao shina lao ni katika Amaleki, Nyuma yako, Benyamini, kati ya watu wako. Kutoka Makiri walishuka makamanda, Na kutoka Zabuloni wao washikao fimbo ya mwandishi.


Na baada ya hayo Samweli akaenda zake kule Rama; naye Sauli akakwea kwenda nyumbani kwake huko Gibea ya Sauli.


Kisha alikuwa akirudi Rama; maana ndipo ilipokuwa nyumba yake; nako ndiko alikowaamua Waisraeli; na huko akamjengea BWANA madhabahu.


Ndipo wazee wote wa Israeli wakakutana pamoja, wakamwendea Samweli huko Rama;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo