Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Hosea 5:7 - Swahili Revised Union Version

7 Wamemtendea BWANA kwa hila; maana wamezaa wana wageni; sasa mwezi huu uandamao utawaangamiza pamoja na mashamba yao.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

7 Wamevunja uaminifu kwa Mwenyezi-Mungu, wamezaa watoto walio haramu. Mwezi mwandamo utawaangamiza, pamoja na mashamba yao.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

7 Wamevunja uaminifu kwa Mwenyezi-Mungu, wamezaa watoto walio haramu. Mwezi mwandamo utawaangamiza, pamoja na mashamba yao.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

7 Wamevunja uaminifu kwa Mwenyezi-Mungu, wamezaa watoto walio haramu. Mwezi mwandamo utawaangamiza, pamoja na mashamba yao.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

7 Wao si waaminifu kwa Mwenyezi Mungu; wamezaa watoto haramu. Sasa sikukuu zao za Mwandamo wa Mwezi zitawaangamiza wao pamoja na mashamba yao.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

7 Wao si waaminifu kwa bwana; wamezaa watoto haramu. Sasa sikukuu zao za Mwandamo wa Mwezi zitawaangamiza wao pamoja na mashamba yao.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

7 Wamemtendea BWANA kwa hila; maana wamezaa wana wageni; sasa mwezi huu uandamao utawaangamiza pamoja na mashamba yao.

Tazama sura Nakili




Hosea 5:7
15 Marejeleo ya Msalaba  

Uniponye, unitoe, Katika mkono wa wageni. Vinywa vyao vyasema visivyofaa, Na mkono wao wa kulia ni mkono wa uongo.


Uinyoshe mikono yako toka juu, uniponye, Unitoe katika maji mengi, kutoka kwa mkono wa wageni,


Sikukuu zenu za mwezi mpya na karamu zenu zilizoamriwa, nafsi yangu yazichukia; mambo hayo yanilemea; nimechoka kuyachukua.


Naam, hukusikia; naam, hukujua; naam, tokea zamani sikio lako halikuzibuka; maana nilijua ya kuwa wewe watenda kwa hila nyingi, nawe umeitwa mkosaji tangu kuzaliwa kwako;


katika kukosa na kumkana BWANA, na katika kugeuka tusimfuate Mungu wetu, tukinena udhalimu na uasi, na kukusudia maneno ya uongo na kuyatoa moyoni.


Bali, kama vile mke amwachavyo mumewe kwa hiana, ndivyo mlivyonitenda mimi kwa hiana, Ee nyumba ya Israeli, asema BWANA.


Maana nyumba ya Israeli na nyumba ya Yuda wamenitenda kwa hiana sana, asema BWANA.


Basi uwaambie, Bwana MUNGU asema hivi; Maneno yangu hayatakawilishwa tena hata moja, bali neno nitakalolinena litatimizwa, asema Bwana MUNGU.


Tena nitaikomesha furaha yake yote, na sikukuu zake, na siku zake za mwandamo wa mwezi, na sabato zake, na makusanyiko yake yote yaliyoamriwa.


naam, sitawaonea rehema watoto wake; kwa maana ni watoto wa uzinzi.


Lakini wao wamelivunja hilo agano kama Adamu; huko wamenitenda mambo ya hiana.


Ole wao! Kwa kuwa wamenikimbia; uharibifu na uwapate! Kwa kuwa wameniasi; ingawa ninataka kuwakomboa, hata hivyo wamenena uongo juu yangu.


Nami nikawakatilia mbali wachungaji watatu katika mwezi mmoja; maana nafsi yangu ilikuwa imechoka kwa ajili yao, na nafsi zao pia walinichukia.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo