Fimbo ya enzi haitaondoka katika Yuda, Wala mfanya sheria kati ya miguu yake, Hata atakapokuja Yeye, mwenye milki, Ambaye mataifa watamtii.
Hosea 10:3 - Swahili Revised Union Version Yakini sasa watasema, Hatuna mfalme; kwa maana hatumchi BWANA; na mfalme huyu je! Aweza kututendea nini? Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Wakati huo watasema: “Hatuna tena mfalme, kwa kuwa hatumchi Mwenyezi-Mungu; lakini, naye mfalme atatufanyia nini?” Biblia Habari Njema - BHND Wakati huo watasema: “Hatuna tena mfalme, kwa kuwa hatumchi Mwenyezi-Mungu; lakini, naye mfalme atatufanyia nini?” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Wakati huo watasema: “Hatuna tena mfalme, kwa kuwa hatumchi Mwenyezi-Mungu; lakini, naye mfalme atatufanyia nini?” Neno: Bibilia Takatifu Kisha watasema, “Hatuna mfalme kwa sababu hatukumheshimu Mwenyezi Mungu. Lakini hata kama tungekuwa na mfalme, angeweza kutufanyia nini?” Neno: Maandiko Matakatifu Kisha watasema, “Hatuna mfalme kwa sababu hatukumheshimu bwana. Lakini hata kama tungelikuwa na mfalme, angeweza kutufanyia nini?” BIBLIA KISWAHILI Yakini sasa watasema, Hatuna mfalme; kwa maana hatumchi BWANA; na mfalme huyu je! Aweza kututendea nini? |
Fimbo ya enzi haitaondoka katika Yuda, Wala mfanya sheria kati ya miguu yake, Hata atakapokuja Yeye, mwenye milki, Ambaye mataifa watamtii.
Huyo Shalumu mwana wa Yabeshi alianza kutawala katika mwaka wa thelathini na tisa wa Uzia mfalme wa Yuda; akatawala muda wa mwezi mmoja katika Samaria.
Waliosema, Kwa ndimi zetu tutashinda; Midomo yetu ni yetu wenyewe, Ni nani aliye bwana juu yetu?
Wasema, Na afanye haraka, aihimize kazi yake, tupate kuiona; na likaribie shauri lake aliye Mtakatifu wa Israeli, tupate kuliona.
Hivyo ndivyo Betheli atakavyowatenda ninyi, kwa sababu ya ubaya wenu mwingi; wakati wa mapambazuko mfalme wa Israeli atakatiliwa mbali kabisa.
Hatarudi tena nchi ya Misri; bali huyo Mwashuri atakuwa mfalme wake; kwa sababu walikataa kurejea.
Yuko wapi sasa mfalme wako, apate kukuokoa katika miji yako yote? Na hao waamuzi wako, uliowanena hivi, Nipe mfalme na wakuu?
Kwa maana wana wa Israeli watakaa siku nyingi bila mfalme, wala mtu mkuu, wala sadaka, wala nguzo, wala naivera, wala kinyago;
Sasa mbona unapiga kelele? Je! Hakuna mfalme kwako, mshauri wako amepotea, hata umeshikwa na uchungu kama mwanamke wakati wa kuzaa?
Basi wale wakapiga kelele, Mwondoshe! Mwondoshe! Msulubishe! Pilato akawaambia, Je! Nimsulubishe mfalme wenu! Wakuu wa makuhani wakamjibu, Sisi hatuna mfalme ila Kaisari.