Akainua macho yake, akamwona Benyamini, nduguye, mwana wa mama yake, akasema, Huyu ndiye ndugu yenu mdogo, mliyeniambia habari zake? Akasema, Mungu akufadhili, mwanangu.
Hesabu 6:25 - Swahili Revised Union Version BWANA akuangazie nuru za uso wake, na kukufadhili; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mwenyezi-Mungu awaangalie kwa wema, na kuwafadhili; Biblia Habari Njema - BHND Mwenyezi-Mungu awaangalie kwa wema, na kuwafadhili; Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mwenyezi-Mungu awaangalie kwa wema, na kuwafadhili; Neno: Bibilia Takatifu Mwenyezi Mungu akuangazie nuru ya uso wake na kukufadhili; Neno: Maandiko Matakatifu bwana akuangazie nuru ya uso wake na kukufadhili; BIBLIA KISWAHILI BWANA akuangazie nuru za uso wake, na kukufadhili; |
Akainua macho yake, akamwona Benyamini, nduguye, mwana wa mama yake, akasema, Huyu ndiye ndugu yenu mdogo, mliyeniambia habari zake? Akasema, Mungu akufadhili, mwanangu.
Unielekee na kunifadhili mimi; Mpe mtumishi wako nguvu zako, Umwokoe mwana wa mjakazi wako.
Akasema, Nitapitisha wema wangu wote mbele yako, nami nitalitangaza jina la BWANA mbele yako; nami nitamfadhili yeye nitakayemfadhili; nitamrehemu yeye nitakayemrehemu.
Basi sasa, Ee Mungu wetu, yasikilize maombi ya mtumishi wako, na dua zake, ukaangazishe uso wako juu ya patakatifu pako palipo ukiwa, kwa ajili ya Bwana.
Na sasa, nawasihi, ombeni fadhili za Mungu, ili atupe neema; ikiwa jambo hili limetoka katika mikono yenu; Je, Atawakubali nafsi zenu? Asema BWANA wa majeshi.
Kwa kuwa torati ilitolewa kwa mkono wa Musa; neema na kweli zilikuja kwa mkono wa Yesu Kristo.
kwa wote walioko Rumi, wapendwao na Mungu, walioitwa kuwa watakatifu. Neema na iwe kwenu na amani itokayo kwa Mungu Baba yetu, na kwa Bwana Yesu Kristo.