Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Malaki 1:9 - Swahili Revised Union Version

9 Na sasa, nawasihi, ombeni fadhili za Mungu, ili atupe neema; ikiwa jambo hili limetoka katika mikono yenu; Je, Atawakubali nafsi zenu? Asema BWANA wa majeshi.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

9 Kwa hiyo sasa enyi makuhani, mwombeni Mungu ili atuhurumie. Ikiwa mnamtolea matoleo ya aina hiyo, je, kweli atakuwa radhi nanyi?

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

9 Kwa hiyo sasa enyi makuhani, mwombeni Mungu ili atuhurumie. Ikiwa mnamtolea matoleo ya aina hiyo, je, kweli atakuwa radhi nanyi?

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

9 Kwa hiyo sasa enyi makuhani, mwombeni Mungu ili atuhurumie. Ikiwa mnamtolea matoleo ya aina hiyo, je, kweli atakuwa radhi nanyi?

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

9 “Basi mwombeni Mungu awe na neema kwetu. Je, kwa sadaka kama hizo kutoka mikononi mwenu, atawapokea?” asema Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

9 “Basi mwombeni Mungu awe na neema kwetu. Je, kwa sadaka kama hizo kutoka mikononi mwenu, atawapokea?” asema bwana Mwenye Nguvu Zote.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

9 Na sasa, nawasihi, ombeni fadhili za Mungu, ili atupe neema; ikiwa jambo hili limetoka katika mikono yenu; Je, Atawakubali nafsi zenu? Asema BWANA wa majeshi.

Tazama sura Nakili




Malaki 1:9
15 Marejeleo ya Msalaba  

Ndipo wakasimama makuhani Walawi, wakawabariki watu; ikasikiwa sauti yao, sala yao ikafika hata makao yake matakatifu, yaani, mbinguni.


Musa akamsihi sana BWANA, Mungu wake, na kusema, BWANA, kwa nini hasira zako kuwaka juu ya watu wako uliowaleta kutoka nchi ya Misri kwa uweza mkuu, na kwa mkono wenye nguvu?


Je! Hezekia, mfalme wa Yuda, na watu wote wa Yuda, walimwua Mikaya? Je! Hakumcha BWANA, na kumwomba BWANA awafadhili; naye BWANA akaghairi, asiyatende mabaya yale aliyoyatamka juu yao? Lakini sisi tuko karibu kujiletea maafa makuu wenyewe.


Lakini ikiwa hao ni manabii, na ikiwa neno la BWANA liko kwao, basi na wamwombe BWANA wa majeshi, kwamba vyombo vile vilivyosalia katika nyumba ya BWANA, na katika nyumba ya mfalme wa Yuda, na hapa Yerusalemu, visiende Babeli.


Inuka, ulalamike usiku, Mwanzo wa mikesha yake; Mimina moyo wako kama maji usoni pa Bwana; Umwinulie mikono yako; Kwa uhai wa watoto wako wachanga wazimiao kwa njaa, Mwanzo wa kila njia kuu.


Lakini hata sasa, asema BWANA, nirudieni mimi kwa mioyo yenu yote, na kwa kufunga, na kwa kulia, na kwa kuomboleza;


Hao makuhani, wahudumu wa BWANA, na walie Kati ya patakatifu na madhabahu, Na waseme, Uwaachilie watu wako, Ee BWANA, Wala usiutoe urithi wako upate aibu, Hata mataifa watawale juu yao; Kwa nini waseme kati ya watu, Yuko wapi Mungu wao?


Naam, ijapokuwa mnanitolea sadaka zenu za kuteketezwa na sadaka zenu za unga, sitazikubali; wala sitaziangalia sadaka zenu za amani, na za wanyama walionona.


Tunajua ya kuwa Mungu hawasikii wenye dhambi; bali mtu akiwa ni mcha Mungu, na kuyafanya mapenzi yake, humsikia huyo.


kwa maana hakuna upendeleo kwa Mungu.


Na ikiwa mnamwita Baba, yeye ahukumuye kila mtu pasipo upendeleo, kwa kadiri ya kazi yake, nendeni kwa hofu katika wakati wenu wa kukaa hapa kama wageni.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo