Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Danieli 9:17 - Swahili Revised Union Version

17 Basi sasa, Ee Mungu wetu, yasikilize maombi ya mtumishi wako, na dua zake, ukaangazishe uso wako juu ya patakatifu pako palipo ukiwa, kwa ajili ya Bwana.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

17 Kwa hiyo, ee Mungu, isikilize sala yangu na maombi yangu mimi mtumishi wako. Kwa hisani yako, uifadhili tena maskani yako iliyoharibiwa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

17 Kwa hiyo, ee Mungu, isikilize sala yangu na maombi yangu mimi mtumishi wako. Kwa hisani yako, uifadhili tena maskani yako iliyoharibiwa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

17 Kwa hiyo, ee Mungu, isikilize sala yangu na maombi yangu mimi mtumishi wako. Kwa hisani yako, uifadhili tena maskani yako iliyoharibiwa.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

17 “Basi Mungu wetu, sasa sikia maombi na dua za mtumishi wako. Ee Bwana, kwa ajili yako angalia kwa huruma ukiwa wa mahali pako patakatifu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

17 “Basi Mungu wetu, sasa sikia maombi na dua ya mtumishi wako. Ee Bwana, kwa ajili yako angalia kwa huruma ukiwa wa mahali pako patakatifu.

Tazama sura Nakili

Swahili Roehl Bible 1937

17 Sasa Mungu wetu, yasikie maombo ya mtumwa wako na malalamiko yake! Uangaze uso wako juu ya Patakatifu pako palipobomolewa, kwa kuwa ndiwe Bwana!

Tazama sura Nakili




Danieli 9:17
20 Marejeleo ya Msalaba  

Lakini uyaelekee maombi ya mtumwa wako, na dua yake, Ee BWANA, Mungu wangu, uisikilize sauti na maombi ya mtumwa wako, aombayo mbele zako leo.


tega sikio lako, macho yako yakafumbuke, upate kuyasikiliza maombi ya mtumishi wako, ninayoomba mbele zako wakati huu, mchana na usiku, kwa ajili ya wana wa Israeli, watumishi wako; hapo ninapoziungama dhambi za wana wa Israeli, tulizozifanya juu yako; naam, mimi na nyumba ya baba yangu tumefanya dhambi.


Umwangazie mtumishi wako uso wako, Na kunifundisha amri zako.


Wengi husema, Nani atakayetuonesha mema? BWANA, utuinulie nuru ya uso wako.


Mungu na atufadhili na kutubariki, Na kutuangazia uso wake.


Njia yake ijulikane duniani, Wokovu wake katikati ya mataifa yote.


Upite na kupaona palipoharibika milele; Adui ameufanya kila ubaya katika patakatifu.


Wewe uchungaye Israeli, usikie, Wewe umwongozaye Yusufu kama kundi; Wewe uketiye juu ya makerubi, utoe nuru.


Ee BWANA, Mungu wa majeshi, uturudishe, Uangaze uso wako nasi tutaokoka.


Ee Mungu, uturudishe, Uangaze uso wako nasi tutaokoka.


Ee BWANA, Mungu wa majeshi, hadi lini Utayaghadhibikia maombi ya watu wako?


Ee Mungu wa majeshi, uturudishe, Uangaze uso wako nasi tutaokoka.


Kwa ajili ya nafsi yangu, kwa ajili ya nafsi yangu, nitatenda haya; je! Litiwe unajisi jina langu? Wala sitampa mwingine utukufu wangu.


Ukaisikia sauti yangu; usifiche sikio lako Ili usisikie pumzi yangu, kwa kilio changu.


Kwa ajili ya mlima Sayuni ulio ukiwa, Mbweha hutembea juu yake.


Ee Bwana, usikie; Ee Bwana, usamehe; Ee Bwana, usikilize, ukatende, usikawie; kwa ajili yako wewe, Ee Mungu wangu; kwa sababu mji wako na watu wako wanaitwa kwa jina lako.


Hata sasa hamjaomba neno kwa jina langu; ombeni, nanyi mtapata; furaha yenu iwe timilifu.


Maana ahadi zote za Mungu zilizopo katika yeye ni Ndiyo; tena kwa hiyo katika yeye ni Amin; Mungu apate kutukuzwa kwa sisi.


Na mji ule hauhitaji jua wala mwezi kuuangaza, kwa maana utukufu wa Mungu huutia nuru, na taa yake ni Mwana-kondoo.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo