Ufunuo juu ya Moabu. Maana katika usiku mmoja Ari wa Moabu umeharibiwa kabisa na kuangamizwa; maana katika usiku mmoja Kiri wa Moabu umeharibiwa kabisa na kuangamizwa.
Hesabu 21:15 - Swahili Revised Union Version Na materemko ya hizo bonde Kwenye kuteremkia maskani ya Ari, Na kutegemea mpaka wa Moabu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema na mteremko wa mabonde unaofika hadi mji wa Ari, na kuelekea mpakani mwa Moabu!” Biblia Habari Njema - BHND na mteremko wa mabonde unaofika hadi mji wa Ari, na kuelekea mpakani mwa Moabu!” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza na mteremko wa mabonde unaofika hadi mji wa Ari, na kuelekea mpakani mwa Moabu!” Neno: Bibilia Takatifu na miteremko ya mabonde inayofika hadi makazi ya Ari, na kuegemea mpakani mwa Moabu.” Neno: Maandiko Matakatifu na miteremko ya mabonde inayofika hadi mji wa Ari na huelekea mpakani mwa Moabu.” BIBLIA KISWAHILI Na materemko ya hizo bonde Kwenye kuteremkia maskani ya Ari, Na kutegemea mpaka wa Moabu. |
Ufunuo juu ya Moabu. Maana katika usiku mmoja Ari wa Moabu umeharibiwa kabisa na kuangamizwa; maana katika usiku mmoja Kiri wa Moabu umeharibiwa kabisa na kuangamizwa.
Kwa hiyo imesemwa katika Kitabu cha Vita vya BWANA, Wahebu katika Sufa, Na bonde za Arnoni,
Maana, moto umetoka Heshboni, Umekuwa Ari ya Moabu, Mwali wa moto umetoka mji wa Sihoni; Wakuu wa mahali palipoinuka Arnoni.
kama walivyonifanyia hao wana wa Esau waishio Seiri, na hao Wamoabi waishio Ari; hata nivuke Yordani niingie nchi tupewayo na BWANA, Mungu wetu.
BWANA akaniambia, Usiwasumbue Wamoabi, wala usishindane nao katika mapigano; kwa kuwa sitakupa katika nchi yake kuimiliki; kwa sababu Ari nimewapa wana wa Lutu kuimiliki.