Akasema ya kuwa atawaangamiza Kama Musa, mteule wake, asingalisimama, Mbele zake na kusimama palipobomoka, Ili aigeuze hasira yake asije akawaangamiza.
Hesabu 11:2 - Swahili Revised Union Version Ndipo watu wakamlilia Musa; naye Musa akamwomba BWANA, na ule moto ukakoma. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Watu wakamlilia Mose, naye akamwomba Mwenyezi-Mungu na moto huo ukazimika. Biblia Habari Njema - BHND Watu wakamlilia Mose, naye akamwomba Mwenyezi-Mungu na moto huo ukazimika. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Watu wakamlilia Mose, naye akamwomba Mwenyezi-Mungu na moto huo ukazimika. Neno: Bibilia Takatifu Watu walipomlilia Musa, akamwomba Mwenyezi Mungu, nao moto ukazimika. Neno: Maandiko Matakatifu Watu walipomlilia Musa, akamwomba bwana, nao moto ukazimika. BIBLIA KISWAHILI Ndipo watu wakamlilia Musa; naye Musa akamwomba BWANA, na ule moto ukakoma. |
Akasema ya kuwa atawaangamiza Kama Musa, mteule wake, asingalisimama, Mbele zake na kusimama palipobomoka, Ili aigeuze hasira yake asije akawaangamiza.
Akasema, Ikiwa sasa nimepata neema mbele zako, Bwana, nakuomba, Bwana, uende kati yetu, maana ni watu wenye shingo ngumu; ukasamehe uovu wetu na dhambi yetu, ukatutwae tuwe urithi wako.
Yamkini BWANA, Mungu wako, atayasikia maneno ya huyo kamanda ambaye mfalme wa Ashuru, bwana wake, amemtuma ili amtukane Mungu aliye hai; na BWANA, Mungu wako atayakemea maneno aliyoyasikia; basi, inua dua yako kwa ajili ya mabaki yaliyobakia.
Ndipo BWANA akaniambia, Hata wangesimama mbele zangu Musa na Samweli, moyo wangu usingewaelekea watu hawa; watupe, watoke mbele za macho yangu, wakaende zao.
Sedekia, mfalme, akamtuma Yehukali, mwana wa Shelemia, na Sefania, mwana wa Maaseya, kuhani, kwa Yeremia, nabii, kusema, Utuombee sasa kwa BWANA, Mungu wetu.
wakamwambia Yeremia, nabii, Twakusihi, maombi yetu yakubaliwe mbele yako, ukatuombee kwa BWANA, Mungu wako, yaani, watu hawa wote waliosalia; maana tumesalia wachache tu katika watu wengi, kama macho yako yatuonavyo;
Kisha Haruni akamwambia Musa, Ee bwana wangu nakusihi sana usituwekee dhambi juu yetu, kwa kuwa tumefanya ya upumbavu, na kufanya dhambi.
Watu wakamwendea Musa, wakasema, Tumefanya dhambi kwa sababu tumemnung'unikia Mungu, na wewe; utuombee kwa BWANA, atuondolee nyoka hawa. Basi Musa akawaombea watu.
Simoni akajibu, akasema, Niombeeni ninyi kwa Bwana, yasinifikie mambo haya mliyosema hata moja.
Maana ilitupasa sisi tuwe na kuhani mkuu wa namna hii aliye mtakatifu, asiyekuwa na uovu, asiyekuwa na waa lolote, aliyetengwa na wakosaji, aliyekuwa juu kuliko mbingu;
Basi ungameni dhambi zenu ninyi kwa ninyi, na kuombeana, ili mpate kuponywa. Sala yake mwenye haki ina nguvu nyingi, na hutenda mengi.
Mtu akimwona ndugu yake anatenda dhambi isiyo ya mauti, ataomba, na Mungu atampa uzima kwa ajili ya hao watendao dhambi isiyo ya mauti. Iko dhambi iliyo ya mauti. Sisemi ya kwamba ataomba kwa ajili ya hiyo.