Lakini Lawi na Benyamini hakuwahesabu miongoni mwao; kwa sababu neno la mfalme limemchukiza Yoabu.
Hesabu 1:47 - Swahili Revised Union Version Lakini Walawi kwa kulifuata kabila la baba zao hawakuhesabiwa katika watu hao. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Lakini Walawi hawakuhesabiwa pamoja na yale makabila mengine, Biblia Habari Njema - BHND Lakini Walawi hawakuhesabiwa pamoja na yale makabila mengine, Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Lakini Walawi hawakuhesabiwa pamoja na yale makabila mengine, Neno: Bibilia Takatifu Hata hivyo, jamaa ya kabila la Lawi hawakuhesabiwa pamoja na wengine. Neno: Maandiko Matakatifu Hata hivyo, jamaa ya kabila la Lawi hawakuhesabiwa pamoja na wengine. BIBLIA KISWAHILI Lakini Walawi kwa kulifuata kabila la baba zao hawakuhesabiwa katika watu hao. |
Lakini Lawi na Benyamini hakuwahesabu miongoni mwao; kwa sababu neno la mfalme limemchukiza Yoabu.
kuanzia aliye na umri wa miaka ishirini na zaidi, wote wawezao kutoka kwenda vitani katika Israeli; wewe na Haruni mtawahesabu kwa kufuata majeshi yao.
lakini uwaweke Walawi wawe juu ya maskani ya ushahidi, na juu ya vyombo vyake vyote, na juu ya vitu vyake vyote; wao wataichukua hiyo maskani, na vyombo vyake vyote; nao wataitumikia, na kupanga hema zao kwa kuizunguka maskani pande zote.
Basi vizazi vya Haruni na Musa, siku hiyo BWANA aliyosema na Musa katika mlima wa Sinai, ni hivi.
Uwahesabu wana wa Lawi kwa kufuata nyumba za baba zao na jamaa zao; kila mwanamume kuanzia umri wa mwezi mmoja na zaidi utawahesabu.
Kwa amri ya BWANA, walihesabiwa kwa mkono wa Musa, kila mtu kwa utumishi wake, na kama mzigo wake ulivyokuwa; ndivyo walivyohesabiwa na yeye, kama BWANA alivyomwagiza Musa.