Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Hesabu 1:3 - Swahili Revised Union Version

3 kuanzia aliye na umri wa miaka ishirini na zaidi, wote wawezao kutoka kwenda vitani katika Israeli; wewe na Haruni mtawahesabu kwa kufuata majeshi yao.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

3 wale wote katika Israeli wanaoweza kwenda vitani, wenye umri kuanzia miaka ishirini na zaidi, mtawaweka katika orodha ya vikosi vikosi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

3 wale wote katika Israeli wanaoweza kwenda vitani, wenye umri kuanzia miaka ishirini na zaidi, mtawaweka katika orodha ya vikosi vikosi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

3 wale wote katika Israeli wanaoweza kwenda vitani, wenye umri kuanzia miaka ishirini na zaidi, mtawaweka katika orodha ya vikosi vikosi.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

3 Wewe na Haruni mtawahesabu kwa migawanyo yao wanaume wote katika Israeli wenye miaka ishirini na kuendelea wanaoweza kutumika katika jeshi.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

3 Wewe na Haruni mtawahesabu kwa migawanyo yao wanaume wote katika Israeli wenye miaka ishirini na kuendelea ambao wanaweza kutumika katika jeshi.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

3 kuanzia aliye na umri wa miaka ishirini na zaidi, wote wawezao kutoka kwenda vitani katika Israeli; wewe na Haruni mtawahesabu kwa kufuata majeshi yao.

Tazama sura Nakili




Hesabu 1:3
16 Marejeleo ya Msalaba  

Naye Yoabu akamtolea mfalme jumla ya hesabu ya watu; nao walikuwa wa Israeli mashujaa elfu mia nane wenye kufuta panga; nao wa Yuda walikuwa watu elfu mia tano.


Wana wa Reubeni, na Wagadi, na nusu kabila ya Manase, watu mashujaa, wawezao kuchukua ngao na upanga, na kupiga upinde, wenye ustadi katika kupigana vita, walikuwa watu elfu arubaini na nne mia saba na sitini, walioweza kwenda vitani.


Tena Amazia akawakusanya Yuda, akawaweka kulingana na nyumba za baba zao chini ya makamanda wa maelfu, na makamanda wa mamia, naam, Yuda pia, na Benyamini; tangu wenye miaka ishirini na zaidi akawahesabu, akawaona kuwa watu wateule elfu mia tatu, wawezao kwenda vitani, waliozoea mkuki na ngao.


Nanyi mtaitunza ile sikukuu ya mikate isiyochachwa; kwa kuwa katika siku iyo hiyo mimi nimeyatoa majeshi yenu katika nchi ya Misri; kwa hiyo mtaitunza siku hiyo katika vizazi vyenu vyote, kwa amri ya milele.


Kila mtu apitaye kwa wale waliohesabiwa tangu huyo ambaye umri wake ni miaka ishirini, au zaidi, atatoa hiyo sadaka ya BWANA.


kichwa beka, maana, nusu shekeli, kwa kadiri ya shekeli ya mahali patakatifu, kwa ajili ya kila mtu aliyepita kwa wale waliohesabiwa, aliyekuwa wa umri wa miaka ishirini au zaidi, kwa ajili ya wanaume elfu mia sita na tatu mia tano na hamsini (603,550).


mizoga yenu itaanguka katika jangwa hili, na wote waliohesabiwa miongoni mwenu, kama jumla ya hesabu yenu, tangu waliopata umri wa miaka ishirini na zaidi, hao walioninung'unikia,


Fanya hesabu ya jumuiya yote ya wana wa Israeli, tangu umri wa miaka ishirini, na zaidi, kwa nyumba za baba zao, hao wote katika Israeli wawezao kutoka kuenenda vitani.


Uwahesabu wana wa Lawi kwa kufuata nyumba za baba zao na jamaa zao; kila mwanamume kuanzia umri wa mwezi mmoja na zaidi utawahesabu.


Hakika yangu hapana mtu mmoja katika wale watu waliotoka Misri, tangu huyo aliyepata umri wa miaka ishirini, na zaidi, atakayeiona hiyo nchi niliyomwapia Abrahamu, na Isaka, na Yakobo; kwa sababu hawakuniandama kwa moyo wote;


Hivi ndivyo vituo vya wana wa Israeli, hapo walipotoka nchi ya Misri kwa vikosi chini ya uongozi wa Musa na Haruni.


tangu waliopata umri wa miaka thelathini na zaidi hata umri wa miaka hamsini, wote waingiao katika utumishi huo, ili kufanya kazi ya hema ya kukutania.


Mtu atwaapo mke mpya, asiende vitani pamoja na jeshi, wala asipewe shughuli juu yake yoyote; akae faragha mwaka mmoja nyumbani mwake, apate mfurahisha mkewe aliyemtwaa.


Nikawaamuru wakati huo, nikawaambia, BWANA, Mungu wenu, amewapa ninyi nchi hii muimiliki, basi vukeni ng'ambo wenye silaha mbele ya ndugu zenu, wana wa Israeli, nyote mlio mashujaa.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo