Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Hesabu 3:15 - Swahili Revised Union Version

15 Uwahesabu wana wa Lawi kwa kufuata nyumba za baba zao na jamaa zao; kila mwanamume kuanzia umri wa mwezi mmoja na zaidi utawahesabu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

15 “Wahesabu wana wa Lawi wote kulingana na koo zao na familia zao, kila mwanamume kuanzia watoto wenye umri wa mwezi mmoja na zaidi.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

15 “Wahesabu wana wa Lawi wote kulingana na koo zao na familia zao, kila mwanamume kuanzia watoto wenye umri wa mwezi mmoja na zaidi.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

15 “Wahesabu wana wa Lawi wote kulingana na koo zao na familia zao, kila mwanamume kuanzia watoto wenye umri wa mwezi mmoja na zaidi.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

15 “Wahesabu Walawi kwa jamaa zao na koo zao. Mhesabu kila mwanaume mwenye umri wa mwezi mmoja au zaidi.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

15 “Wahesabu Walawi kwa jamaa zao na koo zao. Mhesabu kila mwanaume mwenye umri wa mwezi mmoja au zaidi.”

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

15 Uwahesabu wana wa Lawi kwa kufuata nyumba za baba zao na jamaa zao; kila mwanamume kuanzia umri wa mwezi mmoja na zaidi utawahesabu.

Tazama sura Nakili




Hesabu 3:15
17 Marejeleo ya Msalaba  

na wale waliohesabiwa kwa nasaba ya makuhani kufuata nyumba za baba zao, na Walawi, wenye umri wa miaka ishirini na zaidi, katika sehemu yao, kwa kadiri ya zamu zao;


Nawapenda wale wanipendao, Na wale wanitafutao kwa bidii wataniona.


Nenda ukalie masikioni mwa Yerusalemu, ukisema, BWANA asema hivi, Nakukumbuka, hisani ya ujana wako, upendo wa wakati wa kuposwa kwako; Jinsi ulivyonifuata huko jangwani, katika nchi isiyopandwa mbegu.


BWANA alinitokea zamani, akisema, Naam nimekupenda kwa upendo wa milele, ndiyo maana nimekuvuta kwa fadhili zangu.


kuanzia aliye na umri wa miaka ishirini na zaidi, wote wawezao kutoka kwenda vitani katika Israeli; wewe na Haruni mtawahesabu kwa kufuata majeshi yao.


Lakini Walawi kwa kulifuata kabila la baba zao hawakuhesabiwa katika watu hao.


Na hao waliohesabiwa katika Walawi kwa jamaa zao ni hawa; wa Gershoni, jamaa ya Wagershoni; na wa Kohathi, jamaa ya Wakohathi; na wa Merari, jamaa ya Wamerari.


Na hao waliohesabiwa kwao walikuwa elfu ishirini na tatu, kila mwanamume tangu huyo aliyepata umri wa mwezi mmoja, na zaidi; kwa kuwa hawakuhesabiwa katika wana wa Israeli, kwa sababu hawakupewa urithi katika wana wa Israeli.


Basi Musa akawahesabu kama alivyoagizwa na neno la BWANA.


Hao waliohesabiwa kwao, kama hesabu ya wanaume wote, kuanzia umri wa mwezi mmoja na zaidi, hao waliohesabiwa kwao walikuwa elfu saba na mia tano.


Kama hesabu ya wanaume wote, kuanzia umri wa mwezi mmoja na zaidi, walikuwa elfu nane na mia sita, wenye kuhudumu katika mahali patakatifu.


Na hao waliohesabiwa kwao, kama hesabu ya wanaume wote, kuanzia umri wa mwezi mmoja na zaidi, walikuwa elfu sita na mia mbili.


Wazaliwa wa kwanza wote walio wanaume kwa hesabu ya majina, kuanzia umri wa mwezi mmoja na zaidi, katika hao waliohesabiwa kwao, walikuwa elfu ishirini na mbili na mia mbili na sabini na watatu.


Ila Yesu alipoona alichukizwa sana, akawaambia, Waacheni watoto wadogo waje kwangu, msiwazuie; kwa maana watoto kama hawa ufalme wa Mungu ni wao.


na ya kuwa tangu utotoni umeyajua Maandiko Matakatifu, ambayo yaweza kukuhekimisha hata upate wokovu kwa imani iliyo katika Kristo Yesu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo