Danieli 5:27 - Swahili Revised Union Version TEKELI, umepimwa katika mizani nawe umeonekana kuwa umepunguka. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema TEKELI maana yake, wewe umepimwa katika mizani, nawe ukaonekana huna uzito wowote. Biblia Habari Njema - BHND TEKELI maana yake, wewe umepimwa katika mizani, nawe ukaonekana huna uzito wowote. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza TEKELI maana yake, wewe umepimwa katika mizani, nawe ukaonekana huna uzito wowote. Neno: Bibilia Takatifu “Tekeli: Wewe umepimwa katika mizani na kuonekana umepungua. Neno: Maandiko Matakatifu “Tekeli: Wewe umepimwa katika mizani na umeonekana umepungua. Swahili Roehl Bible 1937 Tekel ni kwamba: Umepimwa kwa mizani, ukaoneka kuwa mwepesi. |
Hakika binadamu ni ubatili, Na wenye cheo ni uongo, Katika mizani huinuka; Wote pamoja ni hafifu kuliko ubatili.
Nawe, mwanadamu, ujipatie upanga mkali, kama wembe wa kinyozi ujipatie, ukaupitishe juu ya kichwa chako na ndevu zako; kisha ujipatie mizani ya kupimia, ukazigawanye nywele hizo.
Tena BWANA ametoa amri katika habari zako, ya kwamba asiwepo tena mtu awaye yote mwenye jina lako; toka nyumba ya miungu yako nitakatilia mbali sanamu ya kuchora, na sanamu ya kuyeyusha; nitakufanyia kaburi lako; kwa maana u mbovu.
Maana siku ile itaidhihirisha, kwa kuwa yafunuliwa katika moto; na ule moto wenyewe utaijaribu kazi ya kila mtu, ni ya namna gani.