Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Danieli 5:28 - Swahili Revised Union Version

28 PERESI, ufalme wako umegawanyika, nao wamepewa Wamedi na Waajemi.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

28 PERESI maana yake, ufalme wako umegawanywa kati ya Wamedi na Wapersi.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

28 PERESI maana yake, ufalme wako umegawanywa kati ya Wamedi na Wapersi.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

28 PERESI maana yake, ufalme wako umegawanywa kati ya Wamedi na Wapersi.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

28 “Peresi: Ufalme wako umegawanywa na kupewa Wamedi na Waajemi.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

28 “Peresi: Ufalme wako umegawanywa na kupewa Wamedi na Waajemi.”

Tazama sura Nakili

Swahili Roehl Bible 1937

28 Peresi ni kwamba: Ufalme wako umegawanyika, wakapewa Wamedi na Wapersia.

Tazama sura Nakili




Danieli 5:28
16 Marejeleo ya Msalaba  

Koreshi, mfalme wa Uajemi asema hivi; BWANA, Mungu wa mbinguni, amenipa falme zote za dunia; naye ameniagiza nimjengee nyumba katika Yerusalemu, ulioko Yuda. Basi kila mtu katika ninyi nyote mlio watu wake, BWANA, Mungu wake, na awe pamoja naye, na akwee.


Tazama, nitawaamsha Wamedi juu yao, ambao hawaoni fedha kuwa kitu, wala hawafurahii dhahabu.


Nimeoneshwa maono magumu; atendaye hila anatenda hila, mharibu anaharibu. Panda juu, Ee Elamu; husuru, Ee Umedi; mimi ninakomesha maombolezo yake yote.


Kwa sababu hiyo uovu utakupata; wala hutaweza kuuagua; na msiba utakuangukia; hutaweza kuuondoa; na ukiwa usioujua utakupata kwa ghafla.


Nami nitaleta juu ya nchi ile maneno yangu yote niliyoyanena juu yake, naam, yote yaliyoandikwa ndani ya kitabu hiki, aliyotabiri Yeremia juu ya mataifa haya yote.


Wekeni mataifa tayari juu yake, wafalme wa Wamedi, na watawala wake, na wakuu wake, na nchi yote ya mamlaka yake.


Na sanamu hii kichwa chake kilikuwa ni cha dhahabu safi; kifua chake na mikono yake ni ya fedha; tumbo lake na viuno vyake ni vya shaba;


Na baada yako utainuka ufalme mwingine mdogo kuliko wewe; na ufalme mwingine wa tatu wa shaba, utakaoitawala dunia yote.


Na Dario, Mmedi, akaupokea ufalme, naye umri wake alikuwa na miaka sitini na miwili.


Basi Danieli huyo akafanikiwa katika enzi ya Dario, na katika enzi ya Koreshi, Mwajemi.


Sasa, Ee mfalme, piga marufuku, ukatie sahihi maandiko haya, yasibadilike, kama ilivyo sheria ya Wamedi na Waajemi, isiyoweza kubadilika.


Yule kondoo dume uliyemwona, mwenye pembe mbili, hizo ndizo wafalme wa Umedi na Uajemi.


Katika mwaka wa kwanza wa Dario, mwana wa Ahasuero, wa uzao wa Wamedi, aliyetawazwa kuwa mfalme juu ya milki ya Wakaldayo;


Waparthi na Wamedi na Waelami, nao wakaao Mesopotamia, Yudea na Kapadokia, Ponto na Asia,


Tufuate:

Matangazo


Matangazo