Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

Nahumu 1:14 - Swahili Revised Union Version

14 Tena BWANA ametoa amri katika habari zako, ya kwamba asiwepo tena mtu awaye yote mwenye jina lako; toka nyumba ya miungu yako nitakatilia mbali sanamu ya kuchora, na sanamu ya kuyeyusha; nitakufanyia kaburi lako; kwa maana u mbovu.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

14 Mwenyezi-Mungu ameamuru hivi kuhusu Ninewi: “Hutapata wazawa kulidumisha jina lako. Sanamu zako za kuchonga na za kusubu, nitazivunjavunja nyumbani mwa miungu yako. Mimi nitakuchimbia kaburi lako, maana wewe hufai kitu chochote.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

14 Mwenyezi-Mungu ameamuru hivi kuhusu Ninewi: “Hutapata wazawa kulidumisha jina lako. Sanamu zako za kuchonga na za kusubu, nitazivunjavunja nyumbani mwa miungu yako. Mimi nitakuchimbia kaburi lako, maana wewe hufai kitu chochote.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

14 Mwenyezi-Mungu ameamuru hivi kuhusu Ninewi: “Hutapata wazawa kulidumisha jina lako. Sanamu zako za kuchonga na za kusubu, nitazivunjavunja nyumbani mwa miungu yako. Mimi nitakuchimbia kaburi lako, maana wewe hufai kitu chochote.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

14 Hii ndiyo amri Mwenyezi Mungu aliyoitoa kukuhusu wewe, Ninawi: “Hutakuwa na wazao watakaoendeleza jina lako. Nitaharibu sanamu za kuchonga na sanamu za kusubu zilizopo katika hekalu la miungu yenu. Nitaandaa kaburi lako, kwa maana wewe ni mwovu kabisa.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

14 Hii ndiyo amri bwana aliyoitoa kukuhusu wewe, Ninawi: “Hutakuwa na wazao watakaoendeleza jina lako. Nitaharibu sanamu za kuchonga na sanamu za kuyeyusha ambazo zipo katika hekalu la miungu yenu. Nitaandaa kaburi lako, kwa maana wewe ni mwovu kabisa.”

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

14 Tena BWANA ametoa amri katika habari zako, ya kwamba asiwepo tena mtu awaye yote mwenye jina lako; toka nyumba ya miungu yako nitakatilia mbali sanamu ya kuchora, na sanamu ya kuyeyusha; nitakufanyia kaburi lako; kwa maana u mbovu.

Tazama sura Nakili

Nahumu 1:14
21 Marejeleo ya Msalaba  

Ikawa, alipokuwa akiabudu nyumbani mwa Nisroki, mungu wake, Adrameleki na Shareza wakampiga kwa upanga; wakaikimbilia nchi ya Ararati. Na Esar-hadoni mwanawe akatawala mahali pake.

Naye BWANA akatuma malaika aliyewakatia mbali wapiganaji vita wote, na majemadari, na makamanda, kambini mwa mfalme wa Ashuru. Basi akarudia nchi yake kwa aibu. Naye alipoingia nyumbani mwa mungu wake, baadhi ya wanawe mwenyewe wakamwangamiza humo kwa upanga.

Kumbukumbu lake litakoma katika nchi, Wala hatakuwa na jina mashambani.

Wazawa wake waangamizwe, Jina lao likafutwe katika kizazi cha pili.

Uwe kwangu mwamba wa makazi yangu, Ngome imara ya wokovu wangu. Maana wewe, Ndiwe mwamba wangu na ngome yangu.

Maana nitapita kati ya nchi ya Misri usiku huo, nami nitawaua wazaliwa wa kwanza wote katika nchi ya Misri, wa mwanadamu na wa mnyama; nami nitafanya hukumu juu ya miungu yote ya Misri; Mimi ndimi BWANA.

Kuwakumbuka wenye haki huwa na baraka; Bali jina la mtu mwovu litaoza.

Ufunuo juu ya Misri. Tazama, BWANA amepanda juu ya wingu jepesi, anafika Misri; na sanamu za Misri zinatikisika mbele zake, na moyo wa Misri unayeyuka ndani yake.

Sikieni, ninyi mlio mbali, niliyoyatenda; na ninyi mlio karibu, kirini uwezo wangu.

Tangazeni katika mataifa, Mkahubiri na kutweka bendera; Hubirini, msifiche, semeni, Babeli umetwaliwa! Beli amefedheheka; Merodaki amefadhaika; Sanamu zake zimeaibishwa, Vinyago vyake vimefadhaika.

Kisha badala yake atasimama mmoja, mtu astahiliye kudharauliwa, ambaye hawakumpa heshima ya ufalme; naye atakuja wakati wa amani, naye ataupata ufalme kwa kujipendekeza.

TEKELI, umepimwa katika mizani nawe umeonekana kuwa umepunguka.

Nami nitapaharibu mahali penu palipoinuka, na kuziangusha sanamu zenu za jua, nami nitaitupa mizoga yenu juu ya mizoga ya sanamu zenu; na roho yangu itawachukia.

nami nitakatilia mbali sanamu zako na nguzo zako, zitoke kati yako; wala hutaiabudu tena kazi ya mikono yako.

Nami nitayang'oa maashera yenu, yasiwe kati yako; nami nitaiangamiza miji yako.

Wewe umeifanyia nyumba yako kusudi la aibu, kwa kukatilia mbali watu wengi, nawe umetenda dhambi juu ya roho yako.

Kwa maana nimemwambia ya kwamba nitaihukumu nyumba yake milele, kwa ajili ya ule uovu alioujua; kwa kuwa wanawe walijiletea laana, wala yeye hakuwazuia.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo