Biblia ya mtandaoni

Matangazo


Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya




Danieli 10:9 - Swahili Revised Union Version

Lakini niliisikia sauti ya maneno yake; nami niliposikia sauti ya maneno yake, ndipo nikashikwa na usingizi mzito, na uso wangu umeielekea nchi.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Nilipoisikia sauti yake, nilianguka chini kifudifudi, nikashikwa na usingizi mzito.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Nilipoisikia sauti yake, nilianguka chini kifudifudi, nikashikwa na usingizi mzito.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Nilipoisikia sauti yake, nilianguka chini kifudifudi, nikashikwa na usingizi mzito.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Kisha nikamsikia akisema, nami nilipokuwa nikimsikiliza, nikapatwa na usingizi mzito, nikalala kifudifudi.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Kisha nikamsikia akisema, nami nilipokuwa nikimsikiliza, nikalala kifudifudi, nikapatwa na usingizi mzito.

Tazama sura

Swahili Roehl Bible 1937

Nikasika sauti ya maneno yake, tena papo hapo, nilipoisikia sauti ya maneno yake, nikashikwa na usingizi kabisa, nikaanguka kifudifudi, uso wangu ukaelekea chini.

Tazama sura
Tafsiri zingine



Danieli 10:9
11 Marejeleo ya Msalaba  

Na jua lilipokuwa likichwa usingizi mzito ulimshika Abramu, hofu ya giza kuu ikamwangukia.


BWANA Mungu akamletea Adamu usingizi mzito, naye akalala; kisha akatwaa ubavu wake mmoja, akafunika nyama mahali pake,


Katika ndoto, katika maono ya usiku, Usingizi mzito uwajiapo watu, Katika usingizi kitandani;


Katika mawazo yaliyotoka katika maono ya usiku, Hapo usingizi mzito uwaangukiapo wanadamu.


Nilikuwa nimelala, lakini moyo wangu uko macho, Sikiliza! Mpendwa wangu anabisha! Nifungulie, dada yangu, mpenzi wangu, Hua wangu, mkamilifu wangu, Kwa maana kichwa changu kimelowa umande, Nywele zangu zina manyunyu ya usiku.


Na kumbe, mmoja mfano wa wanadamu akanigusa midomo yangu; ndipo nikafumbua kinywa changu, nikanena, nikamwambia yeye aliyesimama karibu nami, Ee Bwana wangu, kwa sababu ya maono haya huzuni zangu zimenipata tena; hata sikubakia na nguvu.


Basi alipokuwa akisema nami, nilishikwa na usingizi mzito na uso wangu uliielekea nchi; lakini alinigusa, akanisimamisha wima.


Nikasikia, na tumbo langu likatetemeka, Midomo yangu ikatikisika kwa sauti ile; Ubovu ukaingia mifupani mwangu, Nikatetemeka katika mahali pangu; Ili nipate kuingoja ile siku ya dhiki, Kundi lao washambuliao wakweapo juu ya watu.


Alipoondoka katika kuomba kwake, akawajia wanafunzi wake, akawakuta wamelala usingizi kwa huzuni.


Petro na wale waliokuwa pamoja naye walikuwa wamelemewa na usingizi; lakini walipokwisha amka waliuona utukufu wake, na wale wawili waliosimama pamoja naye.


Nami nilipomwona, nilianguka miguuni pake kama mtu aliyekufa. Akaweka mkono wake wa kulia juu yangu, akisema, Usiogope, Mimi ni wa kwanza na wa mwisho,