Amosi 5:24 - Swahili Revised Union Version Lakini hukumu na iteremke kama maji, na haki kama maji makuu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Lakini acheni haki itiririke kama maji, uadilifu uwe kama mto usiokauka. Biblia Habari Njema - BHND Lakini acheni haki itiririke kama maji, uadilifu uwe kama mto usiokauka. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Lakini acheni haki itiririke kama maji, uadilifu uwe kama mto usiokauka. Neno: Bibilia Takatifu Lakini acheni haki itiririke kama mto, na uadilifu uwe kama kijito kisichokauka! Neno: Maandiko Matakatifu Lakini acheni haki itiririke kama mto, na uadilifu uwe kama kijito kisichokauka! BIBLIA KISWAHILI Lakini hukumu na iteremke kama maji, na haki kama maji makuu. |
Laiti ungalisikiliza amri zangu! Ndipo amani yako ingalikuwa kama mto wa maji, na haki yako kama mawimbi ya bahari;
BWANA asema hivi, Fanyeni hukumu na haki, mkamtoe yeye aliyetekwa katika mikono ya mdhalimu; wala msiwatende mabaya mgeni, wala yatima, wala mjane, wala kuwadhulumu, wala msimwage damu ya mtu asiye na hatia katika mahali hapa.
Bwana MUNGU asema hivi; Na iwatoshe ninyi, enyi wakuu wa Israeli; ondoeni dhuluma na unyang'anyi; fanyeni hukumu na haki; acheni kutoza kwenu kwa nguvu katika watu wangu, asema Bwana MUNGU.
Ee mwanadamu, yeye amekuonesha yaliyo mema; na BWANA anataka nini kwako, ila kutenda haki, na kupenda rehema, na kwenda kwa unyenyekevu na Mungu wako!