2 Wakorintho 4:8 - Swahili Revised Union Version Pande zote twateseka, bali hatusongwi; twaona shaka, bali hatukati tamaa; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Daima twapata taabu, lakini hatugandamizwi; twapata mashaka, lakini hatukati tamaa; Biblia Habari Njema - BHND Daima twapata taabu, lakini hatugandamizwi; twapata mashaka, lakini hatukati tamaa; Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Daima twapata taabu, lakini hatugandamizwi; twapata mashaka, lakini hatukati tamaa; Neno: Bibilia Takatifu Twataabika kila upande lakini hatuangamizwi; twaona wasiwasi lakini hatukati tamaa; Neno: Maandiko Matakatifu Twataabika kila upande lakini hatuangamizwi; twaona wasiwasi lakini hatukati tamaa; BIBLIA KISWAHILI Pande zote twateseka, bali hatusongwi; twaona shaka, bali hatukati tamaa; |
bali wao wamngojeao BWANA watapata nguvu mpya; watapanda juu kwa mbawa kama tai; watakimbia, wala hawatachoka; watakwenda kwa miguu, wala hawatazimia.
Maana mtini hautachanua maua, Wala mizabibuni hamtakuwa na matunda; Taabu ya mzeituni itakuwa bure, Na mashamba hayatatoa chakula; Zizini hamtakuwa na kundi, Wala vibandani hamtakuwa na kundi la ng'ombe;
Jaribu halikuwapata ninyi, isipokuwa lililo kawaida ya wanadamu; ila Mungu ni mwaminifu; ambaye hatawaacha mjaribiwe kupita muwezavyo; lakini pamoja na lile jaribu atafanya na mlango wa kutokea, ili muweze kustahimili.
Kwa hiyo napendezwa na udhaifu, na matusi, na matatizo, na adha, na shida, kwa ajili ya Kristo. Maana niwapo dhaifu ndipo nilipo na nguvu.
bali katika kila neno tujipatie sifa njema, kama watumishi wa Mungu; katika subira nyingi, katika mateso, katika shida, katika matatizo;
Kwa maana hata tulipokuwa tumefika Makedonia miili yetu haikupata nafuu; bali tuliteseka kotekote; nje palikuwa na vita, ndani hofu.
laiti ningekuwapo pamoja nanyi sasa, na kuigeuza sauti yangu! Maana naona shaka kwa ajili yenu.
Ndipo Samweli akamwambia Sauli, Mbona umenitaabisha mimi, hata kunipandisha juu? Sauli akajibu, Mimi nimetaabika sana; kwa kuwa hao Wafilisti wananifanyia vita, naye Mungu ameniacha; hanijibu tena, wala kwa manabii, wala kwa ndoto; kwa hiyo nimekuita wewe, ili wewe unijulishe nifanyeje.
Naye Daudi akafadhaika sana; kwa sababu watu walikuwa wakisema kwamba apigwe kwa mawe, kwa maana hao watu wote walisononeka, kila mtu kwa ajili ya wanawe na binti zake; lakini Daudi alijitia nguvu katika BWANA, Mungu wake.
Ndipo Sauli akamwambia yule mchukua silaha zake, Futa upanga wako, unichome nao; wasije watu hawa wasiotahiriwa wakanichoma, na kunisimanga. Lakini huyo mchukua silaha zake akakataa; kwa sababu aliogopa sana. Basi Sauli akautwaa upanga wake, akauangukia.