Basi kulikuwa na vita tena kati ya Wafilisti na Israeli; Daudi akashuka mpaka Gobu, na watumishi wake pamoja naye, akapigana na Wafilisti; naye Daudi akaishiwa na nguvu.
2 Samueli 5:22 - Swahili Revised Union Version Lakini wakapanda hao Wafilisti tena mara ya pili, wakajitawanya bondeni mwa Warefai. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kwa mara ya pili, Wafilisti walifika tena na kujitawanya kwenye bonde la Refaimu. Biblia Habari Njema - BHND Kwa mara ya pili, Wafilisti walifika tena na kujitawanya kwenye bonde la Refaimu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kwa mara ya pili, Wafilisti walifika tena na kujitawanya kwenye bonde la Refaimu. Neno: Bibilia Takatifu Wafilisti walikwea kwa mara nyingine na kusambaa katika Bonde la Warefai. Neno: Maandiko Matakatifu Wafilisti walikwea kwa mara nyingine na kusambaa katika Bonde la Warefai. BIBLIA KISWAHILI Lakini wakapanda hao Wafilisti tena mara ya pili, wakajitawanya bondeni mwa Warefai. |
Basi kulikuwa na vita tena kati ya Wafilisti na Israeli; Daudi akashuka mpaka Gobu, na watumishi wake pamoja naye, akapigana na Wafilisti; naye Daudi akaishiwa na nguvu.
Tena, watatu miongoni mwa wale thelathini waliokuwa wakuu wakashuka, wakamwendea Daudi wakati wa mavuno mpaka pango la Adulamu, na kikosi cha Wafilisti walikuwa wamefanya kambi katika bonde la Warefai.
Naye yule nabii akamjia mfalme wa Israeli, akamwambia, Nenda, kusanya nguvu zako, ujue, na kuangalia ufanyavyo; kwa maana mwakani mfalme wa Shamu atakuja juu yako.
Tena itakuwa kama hapo mvunaji ashikapo mabua ya ngano, na mkono wake ukatapo masuke; tena itakuwa kama hapo mtu aokotapo masuke katika bonde la Warefai.
kisha mpaka ukaendelea karibu na bonde la mwana wa Hinomu, na kufika ubavuni mwa huyu Myebusi upande wa kusini (ndio Yerusalemu); kisha mpaka ukaendelea hata kilele cha mlima ulio pale mkabala wa bonde la Hinomu upande wa magharibi, lililo pale mwisho wa bonde la Warefai upande wa kaskazini;