Lakini Amnoni alikuwa na rafiki, jina lake Yonadabu, mwana wa Shama, nduguye Daudi; naye Yonadabu alikuwa mtu mwerevu sana.
2 Samueli 21:21 - Swahili Revised Union Version Naye huyo alipowatukana Israeli, ndipo Yonathani, mwana wa Shimei, nduguye Daudi, akamwua. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Alipowadhihaki Waisraeli, Yonathani mwana wa Shimei, nduguye Daudi, alimuua. Biblia Habari Njema - BHND Alipowadhihaki Waisraeli, Yonathani mwana wa Shimei, nduguye Daudi, alimuua. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Alipowadhihaki Waisraeli, Yonathani mwana wa Shimei, nduguye Daudi, alimuua. Neno: Bibilia Takatifu Alipowadhihaki Israeli, Yonathani mwana wa Shimea, nduguye Daudi, akamuua. Neno: Maandiko Matakatifu Alipowadhihaki Israeli, Yonathani mwana wa Shimea, nduguye Daudi, akamuua. BIBLIA KISWAHILI Naye huyo alipowatukana Israeli, ndipo Yonathani, mwana wa Shimei, nduguye Daudi, akamwua. |
Lakini Amnoni alikuwa na rafiki, jina lake Yonadabu, mwana wa Shama, nduguye Daudi; naye Yonadabu alikuwa mtu mwerevu sana.
Kulikuwa na vita tena huko Gathi; ambako kulikuwa na mtu mrefu sana, mwenye vidole sita katika kila mkono, na vidole sita katika kila mguu, jumla yake ishirini na vinne; yeye naye alizaliwa kwa Mrefai.
Hao wanne walizaliwa kwake huyo Mrefai wa Gathi; wakaanguka kwa mkono wa Daudi, na kwa mikono ya watumishi wake.
Yuko wapi mfalme wa Hamathi, na mfalme wa Arpadi, na mfalme wa mji wa Sefarvaimu, na wa Hena, na wa Iva?
Naye Yonathani, mjombawe Daudi, alikuwa mshauri, na mtu wa akili, na mwandishi; Yehieli mwana wa Hakmoni alikuwa pamoja na wana wa mfalme;
Wafilisti wakasimama juu ya mlima upande huu, na Waisraeli wakasimama juu ya mlima upande huu, huku bonde likiwa katikati.
Mtumishi wako alimwua simba na dubu pia; na huyu Mfilisti asiyetahiriwa atakuwa kama mmoja wao, kwa sababu amewatukana majeshi ya Mungu aliye hai.