Akambariki, akasema, Abramu na abarikiwe na Mungu Aliye Juu Sana, Muumba mbingu na nchi.
2 Samueli 2:5 - Swahili Revised Union Version Basi Daudi akatuma wajumbe kwa watu wa Yabesh-gileadi, na kuwaambia, Na mbarikiwe ninyi na BWANA, kwa kuwa mmemtendea bwana wenu fadhili hii, yaani Sauli, mkamzika. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema aliwatuma watu huko Yabesh-gileadi na ujumbe: “Mwenyezi-Mungu na awabariki kwa maana mlionesha utii wenu kwa Shauli, bwana wenu, kwa kumzika. Biblia Habari Njema - BHND aliwatuma watu huko Yabesh-gileadi na ujumbe: “Mwenyezi-Mungu na awabariki kwa maana mlionesha utii wenu kwa Shauli, bwana wenu, kwa kumzika. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza aliwatuma watu huko Yabesh-gileadi na ujumbe: “Mwenyezi-Mungu na awabariki kwa maana mlionesha utii wenu kwa Shauli, bwana wenu, kwa kumzika. Neno: Bibilia Takatifu akatuma wajumbe kwa wanaume wa Yabesh-Gileadi, kuwaambia, “Mwenyezi Mungu awabariki kwa kuonesha wema huu kwa kumzika Sauli bwana wenu. Neno: Maandiko Matakatifu akatuma wajumbe kwa watu wa Yabeshi-Gileadi kuwaambia, “bwana awabariki kwa kuonyesha wema huu kwa kumzika Sauli bwana wenu. BIBLIA KISWAHILI Basi Daudi akatuma wajumbe kwa watu wa Yabesh-gileadi, na kuwaambia, Na mbarikiwe ninyi na BWANA, kwa kuwa mmemtendea bwana wenu fadhili hii, yaani Sauli, mkamzika. |
Akambariki, akasema, Abramu na abarikiwe na Mungu Aliye Juu Sana, Muumba mbingu na nchi.
Abramu akamwambia mfalme wa Sodoma, Nimeinua mkono wangu kwa BWANA, Mungu Aliye Juu sana, Muumba mbingu na nchi,
Kwa kuwa umekuja jana tu kwa nini nikusumbue leo, na kukuzungusha huku na huko pamoja nasi nami hapa ninaenda niwezapo kwenda? Rudi wewe, ukawarudishe na ndugu zako; rehema na kweli ziwe pamoja nawe.
Akaenda Daudi, akaitwaa mifupa ya Sauli na mifupa ya Yonathani mwanawe mikononi mwa watu wa Yabesh-gileadi; waliyoiiba katika njia ya Beth-sheani, hapo Wafilisti walipowatungika, katika siku hiyo waliyomwua Sauli huko Gilboa;
Wale wanaume wakamwambia, Tutautoa uhai wetu badala ya uhai wenu, ikiwa hamwitangazi habari ya shughuli yetu hii; kisha itakuwa, wakati BWANA atakapotupa nchi hii, tutakutendea kwa hisani na uaminifu.
Basi wakasema, Ni ipi katika makabila ya Israeli ambayo haikufika mbele ya Bwana huko Mispa.
Kisha Naomi akawaambia wakweze wawili, Nendeni sasa mkarejee kila mmoja nyumbani kwa mamaye; BWANA na awatendee mema ninyi, kama ninyi mlivyowatendea mema hao waliofariki na mimi pia.
Naye Naomi akamwambia mkwewe, Na abarikiwe huyo na BWANA, ambaye hakuuacha wema wake, wala kwa hao walio hai wala kwa waliokufa. Kisha Naomi akamwambia, Mtu huyu ni wa ukoo wetu, mmojawapo wa jamaa yetu aliye karibu.
Akamwambia, Mwanangu, ubarikiwe na BWANA; umezidi kuonesha fadhili zako mwisho kuliko mwanzo, kwa vile usivyowafuata vijana, wawe ni maskini au matajiri.
Ikawa, kama baada ya mwezi mmoja, Nahashi, Mwamoni, akakwea na kupiga kambi juu ya Yabesh-gileadi; na watu wote wa Yabeshi wakamwambia Nahashi, Fanya mapatano nasi, na sisi tutakutumikia.
Nao wakawaambia hao wajumbe waliokuja, Waambieni watu wa Yabesh-gileadi, Kesho, wakati wa jua kali, mtapata wokovu. Basi wale wajumbe wakaenda, wakawaarifu watu wa Yabeshi; nao wakafurahi.
Samweli akamwendea Sauli; naye Sauli akamwambia, Ubarikiwe na BWANA, nimeitimiza amri ya BWANA.
Maana mtu akimwona adui yake, je! Atamwacha aende zake salama? Basi BWANA na akulipe mema kwa haya uliyonitendea leo.