Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

Ruthu 3:10 - Swahili Revised Union Version

10 Akamwambia, Mwanangu, ubarikiwe na BWANA; umezidi kuonesha fadhili zako mwisho kuliko mwanzo, kwa vile usivyowafuata vijana, wawe ni maskini au matajiri.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

10 Boazi akasema, “Mwenyezi-Mungu na akubariki, kwa maana kwa yote unayofanya unaonesha heshima zaidi kuliko uliyoyafanya hapo awali, kwa maana hukuwatafuta vijana maskini au tajiri wakuoe.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

10 Boazi akasema, “Mwenyezi-Mungu na akubariki, kwa maana kwa yote unayofanya unaonesha heshima zaidi kuliko uliyoyafanya hapo awali, kwa maana hukuwatafuta vijana maskini au tajiri wakuoe.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

10 Boazi akasema, “Mwenyezi-Mungu na akubariki, kwa maana kwa yote unayofanya unaonesha heshima zaidi kuliko uliyoyafanya hapo awali, kwa maana hukuwatafuta vijana maskini au tajiri wakuoe.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

10 Akamwambia, “Binti yangu, ubarikiwe na Mwenyezi Mungu. Wema huu wa sasa ni mkuu kushinda hata ule ulioonesha mwanzoni. Hukuwakimbilia vijana, wakiwa matajiri au maskini.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

10 Akamwambia, “Binti yangu, ubarikiwe na bwana. Wema huu wa sasa ni mkuu kushinda hata ule ulioonyesha mwanzoni. Hukuwakimbilia vijana, wakiwa matajiri au maskini.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

10 Akamwambia, Mwanangu, ubarikiwe na BWANA; umezidi kuonesha fadhili zako mwisho kuliko mwanzo, kwa vile usivyowafuata vijana, wawe ni maskini au matajiri.

Tazama sura Nakili

Ruthu 3:10
8 Marejeleo ya Msalaba  

Akasema, Karibu, wewe uliyebarikiwa na BWANA, mbona unasimama nje? Kwa maana nimeiweka nyumba tayari, na nafasi kwa ngamia.

Kisha Naomi akawaambia wakweze wawili, Nendeni sasa mkarejee kila mmoja nyumbani kwa mamaye; BWANA na awatendee mema ninyi, kama ninyi mlivyowatendea mema hao waliofariki na mimi pia.

Naye Boazi akajibu, akamwambia, Nimeelezwa sana yote uliyomfanyia mkweo, tangu alipokufa mumeo; na jinsi ulivyowaacha baba yako na mama yako, na nchi yako uliyozaliwa, ukawafikia watu usiowajua tangu hapo.

Naye Naomi akamwambia mkwewe, Na abarikiwe huyo na BWANA, ambaye hakuuacha wema wake, wala kwa hao walio hai wala kwa waliokufa. Kisha Naomi akamwambia, Mtu huyu ni wa ukoo wetu, mmojawapo wa jamaa yetu aliye karibu.

Na tazama, Boazi akaja kutoka Bethlehemu na kuwaamkia wavunaji, akasema, BWANA akae nanyi. Nao wakamwitikia, BWANA na akubariki.

Akasema, Ama! Ni nani wewe? Akamjibu, Ni mimi, Ruthu, mjakazi wako; uitande nguo yako juu ya mjakazi wako; kwa kuwa ndiwe wa jamaa aliye karibu.

Samweli akamwendea Sauli; naye Sauli akamwambia, Ubarikiwe na BWANA, nimeitimiza amri ya BWANA.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo