2 Samueli 19:32 - Swahili Revised Union Version Naye huyo Barzilai alikuwa mzee sana, alikuwa na umri wa miaka themanini; naye amemlisha mfalme hapo alipokuwapo Mahanaimu; kwa kuwa alikuwa mtu mwenye cheo kikubwa. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Barzilai alikuwa mzee sana, mwenye umri wa miaka themanini. Naye Barzilai alikuwa amemtunza mfalme alipokaa huko Mahanaimu, kwa kuwa alikuwa tajiri sana. Biblia Habari Njema - BHND Barzilai alikuwa mzee sana, mwenye umri wa miaka themanini. Naye Barzilai alikuwa amemtunza mfalme alipokaa huko Mahanaimu, kwa kuwa alikuwa tajiri sana. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Barzilai alikuwa mzee sana, mwenye umri wa miaka themanini. Naye Barzilai alikuwa amemtunza mfalme alipokaa huko Mahanaimu, kwa kuwa alikuwa tajiri sana. Neno: Bibilia Takatifu Basi Barzilai alikuwa mzee sana mwenye umri wa miaka themanini. Alikuwa amempatia mfalme mahitaji alipokuwa anaishi huko Mahanaimu, kwa kuwa alikuwa mtu tajiri sana. Neno: Maandiko Matakatifu Basi Barzilai alikuwa mzee sana mwenye umri wa miaka themanini. Alikuwa amempatia mfalme mahitaji wakati alipokuwa anaishi huko Mahanaimu, kwa kuwa alikuwa mtu tajiri sana. BIBLIA KISWAHILI Naye huyo Barzilai alikuwa mzee sana, alikuwa na umri wa miaka themanini; naye amemlisha mfalme hapo alipokuwapo Mahanaimu; kwa kuwa alikuwa mtu mwenye cheo kikubwa. |
Yakobo akaishi katika nchi ya Misri miaka kumi na saba, basi umri wake Yakobo ulikuwa miaka mia moja na arubaini na saba.
Basi Yusufu akafa, mwenye miaka mia moja na kumi; wakampaka dawa, wakamtia katika sanduku, huko Misri.
Naye mfalme akamwambia Barzilai, Uvuke pamoja nami; nami nitakulisha kwangu huko Yerusalemu.
Na Menahemu akawatoza Israeli fedha hiyo, yaani, matajiri wote wenye mali, kila mtu shekeli hamsini za fedha, ili ampe huyo mfalme wa Ashuru. Basi mfalme wa Ashuru akarejea, wala hakukaa huko katika nchi.
Mali yake nayo ilikuwa ni kondoo elfu saba, na ngamia elfu tatu, na jozi za ng'ombe mia tano, na punda wake mia tano, na watumishi wengi sana; basi hivi mtu huyo alikuwa ni mkuu sana kuliko watu wote wa upande wa mashariki.
Musa alikuwa mtu wa miaka mia moja na ishirini alipokufa; jicho lake halikupofuka, wala nguvu za mwili wake hazikupunguka.
Na huko Maoni kulikuwa na mtu mmoja, ambaye alikuwa na mali yake katika Karmeli; naye yule mtu alikuwa tajiri sana, mwenye kondoo elfu tatu na mbuzi elfu moja; naye alikuwa akiwakata manyoya kondoo wake huko Karmeli.