1 Yohana 2:26 - Swahili Revised Union Version Nimewaandikia haya kuhusu habari za watu wale wanaotaka kuwapoteza. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Nimewaandikieni mambo haya kuhusu wale wanaotaka kuwapotosha nyinyi. Biblia Habari Njema - BHND Nimewaandikieni mambo haya kuhusu wale wanaotaka kuwapotosha nyinyi. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Nimewaandikieni mambo haya kuhusu wale wanaotaka kuwapotosha nyinyi. Neno: Bibilia Takatifu Nawaandikia mambo haya kuhusu wale watu ambao wanajaribu kuwapotosha. Neno: Maandiko Matakatifu Nawaandikia mambo haya kuhusu wale watu ambao wanajaribu kuwapotosha. BIBLIA KISWAHILI Nimewaandikia haya kuhusu habari za watu wale wanaotaka kuwapoteza. |
Kwa sababu hiyo, kwa sababu wameshawishi watu wangu, wakisema, Amani; wala hapana amani; na mtu mmoja ajengapo ukuta, tazama, waupaka chokaa isiyokorogwa vema;
kwa maana watajitokeza Makristo wa uongo, na manabii wa uongo, watatoa ishara na maajabu, wapate kuwadanganya, ikiwezekana, hata hao wateule.
Mtu asiwanyang'anye thawabu yenu, kwa kunyenyekea kwa mapenzi yake mwenyewe tu, na kuabudu malaika, akijitia katika maono yake na kujivuna bure, kwa akili zake za kimwili;
Angalieni mtu asiwafanye mateka kwa elimu yake ya bure na madanganyo matupu, kwa jinsi ya mapokeo ya wanadamu, kwa jinsi ya mafundisho ya awali ya ulimwengu, wala si kwa jinsi ya Kristo.
Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine wataikana imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani;
Lakini watu waovu na wadanganyaji wataendelea, na kuzidi kuwa waovu, wakidanganya na kudanganyika.
Kwa maana wadanganyifu wengi wametokea duniani, wasiokiri ya kuwa Yesu Kristo yuaja katika mwili. Huyo ndiye yule mdanganyifu na mpinga Kristo.