Basi hapo Ezra alipokuwa akiomba na kuungama, akilia, na kujiangusha kifudifudi mbele ya nyumba ya Mungu, kusanyiko kubwa sana la wanaume, wanawake na watoto, kutoka katika Israeli likamkusanyikia; maana watu hao walikuwa wakilia sana.
1 Samueli 30:4 - Swahili Revised Union Version Ndipo Daudi na watu waliokuwa pamoja naye wakapaza sauti zao na kulia, hadi walipokuwa hawana nguvu za kulia tena. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Ndipo Daudi na watu wake walipoangua kilio, wakalia hadi walipoishiwa nguvu. Biblia Habari Njema - BHND Ndipo Daudi na watu wake walipoangua kilio, wakalia hadi walipoishiwa nguvu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Ndipo Daudi na watu wake walipoangua kilio, wakalia hadi walipoishiwa nguvu. Neno: Bibilia Takatifu Hivyo Daudi na watu wake wakapaza sauti na kulia hadi wakaishiwa na nguvu za kulia. Neno: Maandiko Matakatifu Hivyo Daudi na watu wake wakapiga yowe mpaka wakaishiwa na nguvu za kulia. BIBLIA KISWAHILI Ndipo Daudi na watu waliokuwa pamoja naye wakapaza sauti zao na kulia, hadi walipokuwa hawana nguvu za kulia tena. |
Basi hapo Ezra alipokuwa akiomba na kuungama, akilia, na kujiangusha kifudifudi mbele ya nyumba ya Mungu, kusanyiko kubwa sana la wanaume, wanawake na watoto, kutoka katika Israeli likamkusanyikia; maana watu hao walikuwa wakilia sana.
Ikawa, hapo huyo malaika wa BWANA alipoyanena maneno haya, kuwaambia wana wa Israeli wote, ndipo hao watu wakainua sauti zao na kulia.
Basi hao watu wakafika Betheli, wakaketi huko mbele ya Mungu hadi jioni, nao wakainua sauti zao na kulia sana.
Hivyo wajumbe wakafika Gibea ya Sauli, wakasema maneno hayo masikioni mwa watu; na watu wote wakainua sauti zao wakalia.
Basi Daudi na watu wake walipoufikia mji, tazama, ulikuwa umechomwa moto; na wake zao, na watoto wao, wanaume kwa wanawake, wamechukuliwa mateka.
Alipofika, tazama, Eli alikuwa ameketi kitini pake kando ya njia, akingojea; maana moyo wake ulitetemeka kwa ajili ya sanduku la Mungu. Na yule mtu alipoingia mjini, akatoa habari, mji wote ukalia.