Yusufu akaona neema machoni pake, akamtumikia. Naye akamweka kuwa msimamizi wa nyumba yake, na yote yaliyomo akayaweka mkononi mwake.
1 Samueli 2:26 - Swahili Revised Union Version Na yule mtoto, Samweli, akazidi kukua akapata kibali kwa BWANA, na kwa watu pia. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mtoto Samueli aliendelea kukua, akazidi kupendwa na Mwenyezi-Mungu na watu. Biblia Habari Njema - BHND Mtoto Samueli aliendelea kukua, akazidi kupendwa na Mwenyezi-Mungu na watu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mtoto Samueli aliendelea kukua, akazidi kupendwa na Mwenyezi-Mungu na watu. Neno: Bibilia Takatifu Naye kijana Samweli akaendelea kukua katika kimo, akimpendeza Mwenyezi Mungu na wanadamu. Neno: Maandiko Matakatifu Naye kijana Samweli akaendelea kukua katika kimo, akimpendeza bwana na wanadamu. BIBLIA KISWAHILI Na yule mtoto, Samweli, akazidi kukua akapata kibali kwa BWANA, na kwa watu pia. |
Yusufu akaona neema machoni pake, akamtumikia. Naye akamweka kuwa msimamizi wa nyumba yake, na yote yaliyomo akayaweka mkononi mwake.
Rehema na kweli zisiachane nawe; Zifunge shingoni mwako; Ziandike juu ya kibao cha moyo wako.
Yule mtoto akakua, akaongezeka nguvu rohoni, akakaa majangwani hadi siku ile alipotokeza hadharani kwa Israeli.
Yule mtoto akakua, akaongezeka nguvu, amejaa hekima, na neema ya Mungu ilikuwa juu yake.
wakimsifu Mungu, na kuwapendeza watu wote. Bwana akalizidisha kanisa kila siku kwa wale waliokuwa wakiokolewa.
Kwa kuwa yeye amtumikiaye Kristo katika mambo hayo humpendeza Mungu, tena hukubaliwa na wanadamu.
Basi yule mwanamke akamzaa mtoto wa kiume akamwita jina lake Samsoni, mtoto huyu akakua, BWANA akambariki.
Naye BWANA akamwangalia Hana, naye akachukua mimba, akazaa watoto, watatu wa kiume na wawili wa kike. Naye huyo mtoto Samweli akakua mbele za BWANA.
Samweli akakua, naye BWANA alikuwa pamoja naye, wala hakuliacha neno lake lolote lianguke chini.