1 Samueli 18:9 - Swahili Revised Union Version Sauli akamwonea Daudi wivu tangu siku ile. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Tangu siku hiyo, Shauli akawa anamwonea kijicho Daudi. Biblia Habari Njema - BHND Tangu siku hiyo, Shauli akawa anamwonea kijicho Daudi. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Tangu siku hiyo, Shauli akawa anamwonea kijicho Daudi. Neno: Bibilia Takatifu Kuanzia wakati ule na kuendelea Sauli akawa na jicho la wivu juu ya Daudi. Neno: Maandiko Matakatifu Kuanzia wakati ule na kuendelea Sauli akawa na jicho la wivu juu ya Daudi. BIBLIA KISWAHILI Sauli akamwonea Daudi wivu tangu siku ile. |
Tena nikagundua kuwa juhudi zote, na ustadi wote katika kazi, hutokana na mtu kumwonea mwingine wivu. Hayo nayo ni ubatili na kufukuza upepo.
Si halali yangu kutumia vilivyo vyangu kama nipendavyo? Au jicho lako limekuwa ovu kwa sababu ya mimi kuwa mwema?
wizi, uuaji, uzinzi, tamaa mbaya, ukorofi, hila, ufisadi, kijicho, matukano, kiburi, upumbavu.
Ndugu, msinung'unikiane, msije mkahukumiwa. Angalieni, mwamuzi amesimama mbele ya milango.
Ikawa siku ya pili yake, roho mbaya kutoka kwa Mungu ikamjia Sauli kwa nguvu, naye akatabiri ndani ya nyumba. Basi Daudi alikuwa akipiga kinubi kwa mkono wake kama siku zote; naye Sauli alikuwa na mkuki mkononi mwake.
Basi Sauli akaghadhibika sana, na maneno haya yakamchukiza; akasema, Wamempa Daudi makumi elfu, na mimi wamenipa elfu tu; kuna nini tena awezayo kupata, isipokuwa ni ufalme?
Kisha Sauli akasema na mwanawe Yonathani, tena na watumishi wake wote, kwamba wamwue Daudi.