Kwa nini umelidharau neno la BWANA, na kufanya yaliyo mabaya machoni pake? Umempiga Uria, Mhiti, kwa upanga, nawe umemtwaa mkewe awe mke wako, nawe umemwua huyo kwa upanga wa Waamoni.
1 Samueli 15:19 - Swahili Revised Union Version Mbona basi hukuitii sauti ya BWANA, bali ukazirukia nyara ukafanya yaliyo maovu machoni pa BWANA? Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kwa nini basi, hukuitii sauti ya Mwenyezi-Mungu? Kwa nini mkakimbilia nyara na hivyo kutenda jambo ovu mbele ya Mwenyezi-Mungu?” Biblia Habari Njema - BHND Kwa nini basi, hukuitii sauti ya Mwenyezi-Mungu? Kwa nini mkakimbilia nyara na hivyo kutenda jambo ovu mbele ya Mwenyezi-Mungu?” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kwa nini basi, hukuitii sauti ya Mwenyezi-Mungu? Kwa nini mkakimbilia nyara na hivyo kutenda jambo ovu mbele ya Mwenyezi-Mungu?” Neno: Bibilia Takatifu Kwa nini hukumtii Mwenyezi Mungu? Kwa nini ulivamia nyara na kufanya uovu machoni pa Mwenyezi Mungu?” Neno: Maandiko Matakatifu Kwa nini hukumtii bwana? Kwa nini ulivamia nyara na kufanya uovu machoni pa bwana?” BIBLIA KISWAHILI Mbona basi hukuitii sauti ya BWANA, bali ukazirukia nyara ukafanya yaliyo maovu machoni pa BWANA? |
Kwa nini umelidharau neno la BWANA, na kufanya yaliyo mabaya machoni pake? Umempiga Uria, Mhiti, kwa upanga, nawe umemtwaa mkewe awe mke wako, nawe umemwua huyo kwa upanga wa Waamoni.
Akafanya yaliyo maovu machoni pa BWANA, sawasawa na machukizo yote ya mataifa, aliowafukuza BWANA mbele ya wana wa Israeli.
Tena akawapitisha wanawe motoni katika bonde la mwana wa Hinomu; akatazama bao, akabashiri, akafanya uganga, akajishughulisha na hao wenye pepo wa utambuzi, na wachawi; akafanya mabaya mengi machoni pa BWANA, na kumkasirisha.
akafanya yaliyo mabaya machoni pa BWANA, Mungu wake; wala hakujinyenyekeza mbele ya Yeremia nabii aliponena kwa kinywa cha BWANA.
Je! Nyumba hii, iitwayo kwa jina langu, imekuwa pango la wanyang'anyi machoni penu? Angalieni, mimi, naam, mimi, nimeliona jambo hili, asema BWANA.
Musa akawaambia, Kwa nini ninyi sasa kuyakaidi maagizo ya BWANA? Maana halitafanikiwa jambo hilo.
Maana Dema aliniacha, akiupenda ulimwengu huu wa sasa, akasafiri kwenda Thesalonike; Kreske amekwenda Galatia; Tito amekwenda Dalmatia.
Basi watu wakazirukia zile nyara, wakatwaa kondoo, na ng'ombe, na ndama, na kuwachinja papo hapo juu ya nchi, nao wale watu walikuwa wakiwala pamoja na damu.
Sauli akamwambia Samweli, Hakika mimi nimeitii sauti ya BWANA, nami nimemleta Agagi, mfalme wa Waamaleki, tena nimewaangamiza Waamaleki kabisa.